UVCCM sasa waunda kamti kuchunguza mgogoro Arusha!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM sasa waunda kamti kuchunguza mgogoro Arusha!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 2, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Peter Saramba, Arusha
  MAKAO Makuu ya Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), unatarajia kutuma kamati maalumu kuchunguza na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro unaofukuta ndani ya umoja huo mkaoni hapa.

  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema kamati hiyo itakayoongozwa na Naibu wake (Bara), Mfaume Kizigo, itawasili Arusha kati ya kesho au keshokutwa.

  Akizungumza kwa simu juzi, Shigela alisema uamuzi huo unalenga kutafuta kiini cha minyukano ya mara kwa mara kati ya makundi ya vijana mkoani Arusha uliodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

  “Awali, nilipanga kufika Arusha mimi binafsi kufanya ziara wilaya zote kuzungumza na viongozi na vijana wa CCM, lakini nimebadilisha mpango baada ya kuibuka kwa malumbano na matamko mbalimbali yanyotolewa na makundi yanayohasimiana ndani ya UVCCM mkoani Arusha,” alisema Shigela.

  Licha ya Kizigo aliyewahi kuwa Katibu wa UVCCM mkoani Arusha, kamati hiyo ya uchunguzi itajumuisha wajumbe wengine, ambao hakuwa tayari kuwataja kwa sababu anaendelea kufanya majadiliano na viongozi wenzake kuangalia wanaostahili kuwamo.

  Shigela alisema katika mpango wake wa awali uliopaswa kuanza Jumapili iliyopita, angekutana na kujadiliana na viongozi kupitia vikao vya mabaraza ya wilaya na mkoa kabla ya kukutana na vijana wote, lakini akabadilisha baada ya malumbano kupamba moto hadi Katibu wa UVCCM Mkoa, Abdallah Mpokwa, kuhamishiwa makao makuu.

  Mpokwa alihamishwa ghafla wiki iliyopita baada ya kutoa tamko lililodaiwa kumsafisha aliyekuwa Mwenyekiti wake, James Ole Millya, aliyehamia Chadema kwa kile alichodai CCM imepoteza dira na mwelekeo katika kutatua na kusimamia maslahi ya umma.

  Ole Millya anasadikiwa kuwa mfuasi mtiifu wa Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, alijitoa CCM na kuhamia Chadema Aprili 16, mwaka huu akikifananisha chama chake cha zamani na gari lenye pancha lisiloweza kumfikisha katika malengo yake kisiasa.

  Siku chache baada ya kuhamia upinzani, baadhi ya vijana wa CCM wakiongozwa na mjumbe wa Baraza Kuu la vijana Taifa, Mrisho Gambo,waliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kudai Ole Millya aliondoka bila kukabidhi Sh2 milioni zilizochangwa kwa lengo la
  kuanzisha Saccos ya vijana.

  Kwa mujibu wa Gambo aliyeongoza mkutano huo na Kennedy Mpumilwa na Salome Hatibu, alidai fedha hizo zilitolewa na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Felix Mrema na mwenzake wa Arumeru Magharibi, Elisa Mollel, ambao kila mmoja alitoa Sh1milioni mwaka 2008. Mrema alithibitisha yeye na mwenzake kutoa kiasi hicho, lakini akasema haikuwa jukumu lao kufuatilia utekelezaji mradi uliokusudiwa.

  Katika mkutano wao, Gambo na wenzake pia walidai Ole Millya aliondoka bila kukabidhi taarifa ya mapato na matumizi ya zaidi Sh600 milioni uliotokana na mradi wa vyumba 96 vya biashara vinavyomilikiwa na UVCCM
  Mkoa wa Arusha vinayopangishwa kwa wafanyabiashara kwa kodi ya wastani wa Sh150,000 hadi Sh300,000 kwa mwezi.

  Baada ya shutuma hizo, Mpokwa alijitokeza kukanusha Ole Millya kudaiwa kitu chochote na kuwaonya vijana kuacha kujitokeza kutoa matamko aliyoyaita ya uongo yanayoshusha heshima na hadhi ya CCM na viongozi wake mbele ya umma.

  SOSI; Mwananchi.
   
 2. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #2
  May 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hawa waache unafiki juzi Chatanda kasema Arusha hakuna mgogoro.
   
 3. FortJeasus

  FortJeasus JF-Expert Member

  #3
  May 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 568
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Wao wenyewe,akiwemo huyu katibu , walikwishakuweka wazi kuwa walioondoka CCM walikuwa wanakisaidia chama kutekeleza maamuzi ya kujivua magamba.
  Sasa habari za kwenda kutatua mgogoro zinatoka wapi!!
   
Loading...