Uvccm na siasa za kubahatisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvccm na siasa za kubahatisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KESSY FRANCIS, Aug 10, 2012.

 1. KESSY FRANCIS

  KESSY FRANCIS Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  UVCCM NA SIASA ZA KUBAHATISHA

  wakati zoezi la uchukuaji na urudishwaji fomu za uchaguzi UVCCM kufungwa, kumejitokeza wimbi la vijana wengi waliomaliza shahada ya kwanza kati ya mwaka 2008-2012. Wengi wao ni wachanga sana na wepesi katika Siasa za chama na duru za kisiasa za kitaifa. Wengi wao chimbuko Lao na mapenzi yao ya dharura Kama sio wanachama maslahi ilianza wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu (2010) ambapo raisi JK alihitaji vijana wachache watakaozunguka nchi nzima kuomba udhamini na baadaye kuzunguka nchi nzima kwa ajili kwa ajili ya kampeni.

  Hapo ndipo vijana wengi walijitokeza kuzidi uhitaji lakini dhamira ya wengi wao ilikuwa ni posho (pesa),pili wengi waliobali walishauriwa warudi katika majimbo wasaidiane na wabunge na madiwani wa CCM na wengi wao walifanya hivyo. Wengi wao walikuwa aidha M/K wa tawi, katibu, mweka hazina au viongozi wa jumuiya ya CCM katika tawi la CCM chuoni kwao. Kwa sasa asililimia kubwa hawana ajira wamekuwa busy wakipashana habari za maisha, kisiasa kupitia mitandao ya kijamii( facebook, Twitter).

  Waliposikia huu mwaka wa uchaguzi na kuaminishwa kuwa huu ni mwaka wa mavuno kwani viongozi watakaochaguliwa watashiriki kumchagua mgombea wa uraisi 2015, vijana wote walioshiriki Katika mchakato sa kampeni 2010 wakakimbilia kuchukua fomu za uongozi wa juu wa UVCCM taifa.!!!

  Swali ambalo watu wengi wanajiuliza kunanini UVCCM, vijana zaidi ya 20 wanachukua fomu ya Makamu mwenyekiti wa UVCCM?? kwani nafasi hii kiongozi anatoka bara, kwa Nafasi M/K wamechukua watu wasoizidi 6 kutoka visiwani Zanzibar.

  JE ni fikra za pesa za dezo wanazohisi watazipata katika mchakato wa kumpata mgombea wa uraisi 2015?? Au jengo jipya na la kisasa la UVCCM ?? au ni ombwe la uongozi uliopo sasa la UVCCM linatoa mwanya wa kila Kijana ahisi anauwezo wa kuongoza jumuiya hii muhimu ya chama?? Au wanadhamira ya kweli inayowasukuma ya uzalendo katika mioyo yao??

  Au wanatumika kwa maslahi ya watu binafsi?? Je wagombea wanajua vijana wa nchi hii wanataka kuona MWANGA BORA katika maisha kupitia UVCCM mathubuti?? Je wanayafahamu matatizo ya sasa ya kiuongozi yanayoikondesha na kutishia kuiuwa UVCCM?? Je wanamajibu gani?? Na je majibu hayo ni kweli yataiponya jumuiya hii muhimu?

  Naona wengi wao ( wagombea) wamejeuka kuwa KASUKU wa mjini, kazi kuimba Wimbo za wazee wao na Siasa zulizochoka na zisizo na utekelezaji za Siasa za makundi zenye kiitikio maarufu cha KUJIVUA GAMBA! Hapa hatuitaji kusikia sera za makundi, ukabila, ukanda, tunataka kusikia utaifanyia nini UVCCM Kama utapata nafasi hiyo au tuseme kauli zenu za KUCHAFUANA zanadhihirisha kwa namna gani hamjakomaa na kupevuka kisiasa??

  Mchujo bado tayari mmeshaanza kukashifiana!! Karne ya ishirini na moja Kijana unakuwa injinia na makandarasi wa unafki, fitna, majungu na uzandiki badala ya sera?? Binafsi nashangaa, kwanza tupeni sifa zenu, elimu yenu, uzoefu na weledi wenu.
  Wengi wenu hamstaili hata kugombea uenyekiti wa mtaa wala balozi wa nyumba kumi.

  UVCCM inahitaji mabadiliko makubwa ya KISERA, KIMUUNDO, na KIMKAKATI ili iweze kupambana na Siasa za ushindani! UVCCM inahitaji kiongozi ambaye

  1. Atatoa uongozi uliotukuka ( provide leadership)
  2. Anakijua chama vizuri na amewahi kuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali kuanzia chini
  3. Awe mzalendo
  4. Awe anaijua TZ na watu wake
  5. Anajiheshimu na kuheshimika
  6. Awajue vijana wa TZ na matatizo yao
  7. Awe tayari kujifunza na kuelekezwa
  8. Awe tayari kukosolewa
  9. Awe tayari kutumika na na kutetea maslahi ya vijana popote pale alipo.
  10. Msukumo wa kuwania uongozi uwe ni kusaidia vijana
  11. Awe tayari kusimamia maslahi a umma kuhakikisha maslahi ya vijana na watanzania hayachezewi na kupokonywa
  12. Aje na programu mahususi zinazotekelezeka kumkwamua Kijana hapo alipo kwenda mbele zaidi kimaendeleo.

  ...............itaendelea ..................

  Sent from my iPhone ( Kessy)
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Well Said Kessy, ni kweli wengi ambao wamechukua fomu wametokea katika mkumbo huo huo ambao umeuzungumzia na wengine ili kupata majukwaa ya kuzungumzia wamekuwa hawakauki Malumbano ya Hoja ITV yote hiyo ikiwa ni kutafuta kujulikana ili waweze kutimiza malengo yao....Kuhusu uwezo wa kujenga hoja na kufanya uchambuzi yakinivu ni tatizo kubwa ukiwasikiliza wanapoongea wengi wao ni watupu sana kiasi kwa unajiuliza either wamemeza wanayoyaaongea na siyo kuyaelewa.Katika List ambayo wametuchukua fomu za uongozi ni Asenga na Matefu ila kwa kifupi wachawawapitishe ili wakimbizwe na Makamanda. Si unaona Kazi nzuri ya Kamanda Heche na Munishi wanaifanya kwenye M4C sasa hawa kula kula wataweza?
  Mytake: Tatizo linalowasumbua hawa madogo ni Ajira sasa wengi wanatumia hii uongozi kwenye vyama kama vichaka.
   
 3. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unaonekana umetumwa na Assenga na Matefu. Haumpati mtu hapa
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  PPM Linalotumwa ni Jini siyo binadamu!Peleka ***** wako kwa magamba wenzako.
   
 5. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ya magamba tunawaachia wenyewe leo wajimwage humu jamvini na ukilaza wao, endeleeni kujadili yetu macho maana tukisema neno utasikia oooh chadema mnamatatizo haya topic yenu jimwageni.
   
Loading...