UVCCM: Makamba ajitafakari ikiwezekana awapishe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM: Makamba ajitafakari ikiwezekana awapishe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 23, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, ametakiwa kujitafakari upya na ikiwezekana aachie ngazi ili awapishe wengine waongoze.

  Kauli hiyo imetolewa na mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, kutoka mkoani Mara, Anthony Mtaka, wakati wa kikao cha viongozi vijana wa chama hicho Mkoani Dodoma.

  Alisema umefika wakati kwa Makamba na viongozi wenzake wa sekretarieti ya chama hicho kutafakari wanavyomsaidia Rais Jakaya Kikwete.

  "Nawataka makada wa CCM akiwamo Makamba waeleze wanamsaidiaje rais katika utendaji wao wa kazi za chama na wajikosoe na kama haitoshi wajitoe," alisema.

  Mtaka alisema viongozi hao wakijikosoa na kubaini upungufu wao wanaweza kumshukuru Rais Kikwete kwa kuwapa nyadhifa hizo na kumwambia wanajitoa kwa sababu ya kushindwa kuwajibika ipasavyo.

  Alisema kwa kufanya hivyo watakuwa wamemsaidia sana rais katika kurahisha utendaji wake wa kazi, kwani ndani ya chama kuna Wana CCM wengi wanaoweza kushika nyadhifa hizo.

  My take: Big up vijana, kwa spidi hii mnaweza kufika lakini lazima kutakuwa na majeruhi wengi miongoni mwenu.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa UVCCM hawawezi kuwa na sauti baada ya uchaguzi kwa hiyo wanayoyaongea sasa ni upepo usovuma! Mbona kwenye tamko rasmi hilo halikuwemo? tafakari
   
Loading...