Vijana wa UVCCM na BAVICHA wamekuwa na uelewa mdogo sana kiasi kwamba wamefikia hatua ya kuwaza nchi imegawanyika vipande viwili chama tawala na CHADEMA + UKAWA. Kila anayekosoa serikali ya chama cha mapinduzi UVCCM humwita mpinzani au UKAWA na kila anayeipongeza serikali na CCM BAVICHA + UKAWA humwita mawazo mgando ya chama kilicho chakaa CCM, wameshindwa kuelewa kuwa nchi hii ina watu milioni kadha wasiokuwa wanachama wa chama chochote cha siasa.
UVCCM walipoona watu wanakosoa approach mbaya ya Mh. Makonda kuhusu madawa ya kulevya walitangaza kuandaa maandamano ya kumuunga mkono wakimaanisha yupo sahihi na wanaomkosoa wote ni wapinzani wa serikali ya CCM, sasa nataka kujua tarehe rasmi ya hayo maandamano, je kumuunga mkono wanakubaliana na Makonda kuwa alikuwa sahihi na wote waliomkosoa hawakuwa sahihi? Je hata Waziri Mkuu hayuko sahihi?
Tuambieni tarehe ya maandamano UVCCM