UVCCM: Kingunge ndiye mwasisi wa uasi na usaliti ndani ya CCM

Massivve

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
274
368
Kingunge-Ngombale-Mwiru-300x220.jpg

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umemtaka mwanasiasa mkongwe kingunge nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, kunyamaza kwani yeye ndiye mwasisi wa uasi na usaliti ndani ya chama hicho tawala kabla ya kuamua kujiondoa mwaka 2015.

Akizungumza jana Kaimu Katiba Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema kauli na shutuma zilizotolewa na Mzee Kingunge akiwatuhumu Mwenyekiti mstaafu wa CCM Dk. Jakaya Kikwete , Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akidai wameshiriki uasi na usaliti katika uteuzi wa mgombea urais mwaka 2015.

Shaka alisema wakati umefika kwa Kingunge kukaa kimya, ili aweze kuleta wajukuu pamoja na kutubu kwa Mungu asiyemuamini.

“UVCCM tunajua fika Mzee Kingunge haamini uwepo wa Mungu ndiyo maana anakuwa jasiri na mahiri wa kuongopa , kama ni uasi na usaliti yeye ndiye bingwa wa kuchongea wenzake kwa siasa za majungu, alichochea kufukuzwa kwa Mzee Aboud Jumbe akishirikiana na kina Seif Sharif Hamad, hakuogopa aliisaliti hata Serikali ya Mwalimu Nyerere ikwame,” alidai Shaka.

Akijibu hoja na madai ya kwamba vigogo hao watatu walikiuka na kuvunja taratibu za vikao katika uteuzi, Shaka alisema hakuna kiongozi wa CCM aliyevuruga taratibu ila kilichofanyika ni kuhakikisha mgombea yeyote anayeteuliwa anatokana na misingi na maadili ya chama hicho.

“Chama chetu mapema kabisa kiliweka msimamo bayana, mgombea atakayebainika kutumia rushwa, anayegawa fedha na mwenye tuhuma za ufisadi au aliyekosa maadili ya uongozi , hateuliwi kuwa mgombea urais na kupeperusha bendera ya CCM, Kingunge na wenzake walifikiri mzaha mwisho wakajionea umadhubuti wa CCM,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
 
Ukiwa shabiki wa UKAWA unakuwa unaishi maisha magumu sana kisaikolojia, yaani tangu mwaka unaanza mpaka unaisha wewe kila siku ni kutukana , KULALAMIKA, KULIALIA, KUKOSOA, Serikali ikifanya zuri linakuumiza. Yataka moyo

kazi ya upinzani ni nini ili nami nijue
 
Huyu mzee hana aibu kabisa, eti anaibukia Upinzani akiwa kachoka kifikra baada ya kuipotezea muda wake ccm.
 
Nyie UVCCM mwe na adabu huyu mzee ni babu yenu wala si size yenu ameingia katika siasa kabla wazazi wenu hawajazaliwa.
 
Hapo walikaa pamoja wakala zao buku saba saba maisha yakasonga wakaamua na wao waseme neno..!
Siasa za nchi hii ni chuki na visasi.
 
Wameibukia kwa Kingunge, tena kwa kuzungumzia mambo yaliyotokea mwaka juzi wakati kuna suala lililopo sasa linalohusu SHUTUMA ya WIZI wa CHETI cha taaluma inayomkabili Mh. Daudi Albert Bashite, wamekaa kimya. Na huyu Shaka amerudi lini toka Mombasa.
 
Nyie UVCCM mwe na adabu huyu mzee ni babu yenu wala si size yenu ameingia katika siasa kabla wazazi wenu hawajazaliwa.
Mzee naye atulie la sivyo atakosewa adabu na wajukuu zake kila siku
 
Huyu Shaka anaejua uwepo wa Mungu mbona ya Makonda kaufyata? Rafiki we.
 
tatizo sio uasi ni demokrasia kila mtu ana uhuru wa kuamua kile anachofikiri kuwa sahihi, na nyie vijana ccm umeikuta juzi tu huyo mzee alianza nayo toka enzi ya tanu hata baba zenu hawajazaliwa, msijifanye mnakijua hicho chama sana kuliko huyo mzee
 
Ukiwa shabiki wa UKAWA unakuwa unaishi maisha magumu sana kisaikolojia, yaani tangu mwaka unaanza mpaka unaisha wewe kila siku ni kutukana , KULALAMIKA, KULIALIA, KUKOSOA, Serikali ikifanya zuri linakuumiza. Yataka moyo

kazi ya upinzani ni nini ili nami nijue
kuvamia vituo vya televishen
 
Huyu mzee hana aibu kabisa, eti anaibukia Upinzani akiwa kachoka kifikra baada ya kuipotezea muda wake ccm.
He is MAN who stands by his PRINCIPLES no matter what
I doubt that you know what that means
numb skull
 
He is MAN who stands by his PRINCIPLES no matter what
I doubt that you know what that means
numb skull
Principles kwamba unakaa mahali kwa ajili ya chakula na kwamba pindi unaponyanganywa hicho chakula basi unakaidi na kuhama, na kuanza kutukana ulikokuwa!
 
Ukiwa shabiki wa UKAWA unakuwa unaishi maisha magumu sana kisaikolojia, yaani tangu mwaka unaanza mpaka unaisha wewe kila siku ni kutukana , KULALAMIKA, KULIALIA, KUKOSOA, Serikali ikifanya zuri linakuumiza. Yataka moyo

kazi ya upinzani ni nini ili nami nijue
Ni hayo uliyoyasema.
 
Back
Top Bottom