kilombero yetu
JF-Expert Member
- May 6, 2011
- 1,004
- 117
UVCCM WATANGAZA VITA NA WANAOTAKA KUICHAFUA JUMUIYA.
Tunapenda kuwajuilisha kwa masikitiko makubwa kuwa Leo alasiri kupitia mtandao mmoja wa kijamii ulisambazwa taarifa ya kihuni na upotoshaji ikiihusisha Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa (UVCCM)dhidi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano Mheshimiwa January Yussuf Makamba.
Tungependa ifahamike kuwa UVCCM haijawahi kuandika wala kujiwa na wazo la kuandika mambo ya kipuuzi na uzushi yaliyoandikwa kwenye taarifa ya mtandao huo na kutoa shutuma zenye taaswira ya unafiki na uzandiki na upotoshaji kwa lengo la kuipaka matope jumuiya yetu mbele ya jamii.
UVCCM haijawahi kufanya kikao chochote cha kikatiba na kujadili suala lolote kuhusu mwenendo wa Waziri yeyote katika Serikali ya awamu ya tano au kushindikiza Serikali imchukulie hatua zozote waziri mhusika.
Aidha Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka hajawahi kutoa tamko lolote linalohusisha jina la Waziri January na tuhuma yoyote ya kutunga uongo, kuamini hatimaye kuueneza katika jamii.
Kutwa nzima jana Kaimu Katibu Mkuu Shaka amekuwa akishiriki maziko ya marehemu Mzee Seleman Khalifan Kikwete katika kijiji cha Msoga jimbo la Chalinze hadi jioni alipoona taarifa hiyo ilioandikwa na kundi la wahuni na kusambazwa.
Tunatambua zipo juhudi na wapo mamluki majeruhi wachache wanaopania kila uchao kutaka aidha kuwagawa wana jumuiya , kuivunjia heshima taasisi yetu na viongozi wenye staha mbele ya jamii na mpasuko na kugombanisha watu kwa sababu wanazozijua wao na mabwana wanaowatumikia.
Nichukue nafasi hii kukanusha kwa sauti ya juu kwamba UVCCM wala ofisi ya Kaimu Katibu Mkuu haihusiani na taarifa inayosambazwa na maadui ambao muda si mrefu watajulikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.
UVCCM tunawaonya na kuwatahadharisha wale wote wenye fikra za kutukwamisha , wajue kuwa mradi wao wa kuwa mawakala wa mafisadi hautafanikiwa wala hautawasaidia kwa wakati huu. Tunawahakikishia UVCCM ni taasisi kubwa hivyo hili na jengine la kutaka kutuchafua tutalikomesha muda mfupi toka leo kwa mujibu sheria.
Tunawaomba radhi nyote kwa usumbufu mliopata
Tunawakaribisha ofisini wakati wowote linapotokea jambo la kutaka ufafanuzi zaidi ama wasilianeni na
Abubakar asenga
Kaimu Katibu Idara ya Hamasa, Sera, Utafiti na Mawasiliano.
Simu 0715429738
SAUTI YA VIJANA NI SAUTI YA UMMA.
Hapa kazi tu