PreGE2025 UVCCM Dodoma: Vyama vya upinzani havina uchumi wa kuhudumia wananchi

PreGE2025 UVCCM Dodoma: Vyama vya upinzani havina uchumi wa kuhudumia wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,410
Reaction score
4,988
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Abdulhabib Mwanyemba, amesema kuwa vyama vya upinzani havina uwezo wa kushika dola kutokana na kutokuwa na misingi imara ya kiuchumi ya kuwahudumia wananchi. Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiamini CCM kwa kuwa ndicho chama chenye dira ya kweli ya maendeleo.

Akiwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kwa baadhi ya wilaya za mkoa huo, Mwanyemba alisisitiza kuwa CCM haiwahangaishi wananchi kwa michango ya mara kwa mara, kwani inaamini kuwa raia wanapaswa kutumia muda wao katika shughuli za kujiletea maendeleo badala ya kuwa sehemu ya maombi ya misaada yasiyo na tija.

Vifaa hivyo vya ujenzi ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoweka pamoja na kamati ya utekelezaji ya mkoa, kufuatia ziara yao ya kutembelea wilaya zote za Dodoma. Lengo kuu ni kusaidia kukamilisha miradi ya ujenzi wa nyumba za UVCCM katika wilaya husika.

Katika awamu ya kwanza ya zoezi hilo, wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Chamwino, na Bahi zimepokea vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi 500,000 kwa kila wilaya, fedha ambazo zimetokana na mapato ya ndani ya mkoa.

Mwanyemba pia ameahidi kuwa utaratibu huo utaendelea hadi wilaya zote zitakapofikiwa, huku akiahidi motisha kwa zile zitakazojitokeza kwa bidii zaidi katika kukamilisha ujenzi wa miradi hiyo.

----
Maoni ya wadau
Jukumu la msingi la kuhudumia wananchi kupitia huduma za afya, elimu, miundombinu na ustawi wa jamii ni la serikali na si chama chochote cha siasa.

Serikali hupewa mamlaka na wananchi kupitia sanduku la kura, si kwa uwezo wa kifedha wa chama fulani.

Kupima uwezo wa kuongoza kwa kigezo cha uwezo wa kifedha wa chama ni kupotosha maana halisi ya uongozi wa kidemokrasia.

Mwamba kakengeuka sana.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dodoma Abdulhabib Mwanyemba amesema hakuna chama chochote cha upinzani kitakachoweza kushika dola kwa kuwa havina uchumi wakuwahudumia wananchi huku akiwataka Watanzania kuendelea kuiamini CCM.

Mwanyemba ameyasema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya ujenzi kwa ajili ya muendelezo wa nyumba za UVCCM Wilaya zilizopo ndani ya Mkoa wa Dodoma.

Amesema “Chama chetu haikihitaji kusumbua wananchi kwaajili ya kuchangisha, changisha kwa sababu tunaamini wananchi wanatakiwa wakafanye mambo yao binafsi yakujikuza kiuchumi, ni kweli tunaweza kuendeshwa na chama ambacho hata kujitegemea hakiwezi ,”

Hata hivyo vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa mwenyekiti pamoja na kamati ya utekelezaji mkoa katika ziara yao waliyoifanya mkoa mzima juu ya kuzisaidia wilaya kufanikisha juhudi zao za kukamilisha nyumba hizi kupitia mchango wa vifaa vya ujenzi.

Wilaya ambazo zimekabidhiwa vifaa vya ujenzi kwa awamu ya kwanza ni Mpwapwa, Kongwa, Chamwino na Bahi huku kila wilaya ikipewa vifaa vyenye thamani ya Tsh 500,000 kupitia mapato ya ndani ya mkoa.

Aidha Mwenyekiti huyo ameahidi kuendelea na utaratibu huu wa mkoa kuzipa nguvu wilaya zilizobaki na kutoa motisha zaidi kwa wilaya itakayoonyesha juhudi katika kukamilisha ujenzi.
Ccm hawana pesa wanazo kodi zetu.
 
Huwa hii nchi kuendelea ni kazi.. kijana kwenye fikra baada ya miaka kadhaa utamiona kapewa position kubwa ya kiutawala na maamuzi.
Mf: uwaziri, ukurugenzi
Unategemea nini?!
 
Amewapa vizuri kwasababu ccm uchumi wanao miaka nenda miaka rudi. Wanayo viwanja
Samora
Sokoine
Jamhuri moro
Jamhuri Dom
CCM kirumba mza
So jamaa wana uchumi mkubwa sana. Wao ndio wananipa pesa gavoo
 
Nilivyoona tu ni kobazi nikajua asilimia 80 lazima atapike pumba....

Awamu hii sijui imekubwa na nn. Tukisema tunaambiwa chuki za kidini.
 
Jukumu la msingi la kuhudumia wananchi kupitia huduma za afya, elimu, miundombinu na ustawi wa jamii ni la serikali na si chama chochote cha siasa.

Serikali hupewa mamlaka na wananchi kupitia sanduku la kura, si kwa uwezo wa kifedha wa chama fulani.

Kupima uwezo wa kuongoza kwa kigezo cha uwezo wa kifedha wa chama ni kupotosha maana halisi ya uongozi wa kidemokrasia.

Mwamba kakengeuka sana.
 
Vipi baba yake Diwani Mzee Mwanyeba atamuachia Udiwani kata ya Viwandani?
 
Back
Top Bottom