UVCCM Arusha walitaka Jeshi la Polisi limkamate Lema

UVCCM Arusha walitaka Jeshi la Polisi limkamate Lema

Urio kimiroI

Senior Member
Joined
Jan 2, 2016
Posts
146
Reaction score
74

Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arusha mjini Martin Munisi amelitaka jeshi la polisi kumkamata Mara moja mbunge wa jimbo la Arusha mjini Chadema God bless Lema kwa kitendo chake cha kusema Mh raisi atakufa kabla ya 2020 kama hatawasikuliza wao chadema Mwenyekiti Martin Munisi ameyasema hayo jioni hii wakati akihojiwa na Radio Sun Rise ya jijini Arusha

Eidha mwkt Munisi amelitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi wa mikutano iliyokatazwa na inayotakiwa maana lema anafanya mikutano ya chadema na siyo mikutano ya mbunge mikutano ya mbunge hulenga kuzungumzia ahadi za mbunge alizotekeleza atakazotekeleza na kuhamasisha maendeleo ila kinyume chake Lema yeye anasema wananchi wataingia barabarani maana hali ni mbaya mara raisi takufa kabla ya 2020

haya ni maneno yasiyovumilika hata kidogo kwenye jamii iliyostaharabika nivizuri jeshi letu likamhoji lema kuhusu kumzushia au kutabiri kifo Kwa mwkt wetu wa chama taifa na na rais wetu .Nakwavile Lema hana agenda nalitaka jeshi la polisi kuzuia mikutano yake kama wasipozuia sidhani kama vijana wa ccm na wananchi wapenda nchi yao watakuwa tayari kuvumilia matusi ya lema kwa Mh rais, wetu mpendwa.

Chanzo: Muungwana
 
Watanzania sasa tumeamua kufanya kazi za pwagu na pwaguzi tunazoagizwa na ccm
 
POLISI ARUSHA WALIMTAKA JESHI LA LEMA LIMKAMATE UVCCM.
msiniulize maswali, napenda ujinga wenye faida.😱
 
haa haa kwa hiyo jeshi la polis limetii agizo la uvccm? haaa haaa...
 
Hana lolote, kanajipendekeza tu walau akumbukwe kwenye teua teua
 
Ndio maana anataka tumuombee anajua 2020 atoboi Lema bwana
 
Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arusha mjini Martin Munisi amelitaka jeshi la polisi kumkamata Mara moja mbunge wa jimbo la Arusha mjini Chadema God bless Lema kwa kitendo chake cha kusema Mh raisi atakufa kabla ya 2020 kama hatawasikuliza wao chadema Mwenyekiti Martin Munisi ameyasema hayo jioni hii wakati akihojiwa na Radio Sun Rise ya jijini Arusha

Eidha mwkt Munisi amelitaka jeshi la polisi kutoa ufafanuzi wa mikutano iliyokatazwa na inayotakiwa maana lema anafanya mikutano ya chadema na siyo mikutano ya mbunge mikutano ya mbunge hulenga kuzungumzia ahadi za mbunge alizotekeleza atakazotekeleza na kuhamasisha maendeleo ila kinyume chake Lema yeye anasema wananchi wataingia barabarani maana hali ni mbaya mara raisi takufa kabla ya 2020

haya ni maneno yasiyovumilika hata kidogo kwenye jamii iliyostaharabika nivizuri jeshi letu likamhoji lema kuhusu kumzushia au kutabiri kifo Kwa mwkt wetu wa chama taifa na na rais wetu .Nakwavile Lema hana agenda nalitaka jeshi la polisi kuzuia mikutano yake kama wasipozuia sidhani kama vijana wa ccm na wananchi wapenda nchi yao watakuwa tayari kuvumilia matusi ya lema kwa Mh rais, wetu mpendwa.

Chanzo: Muungwana
Niliwahi kumwandikia Kubenea baada ya kupata ubunge.
Kubenea amepitia madhila mengi katika uandishi wake na hata kuingia kwake ndani ya siasa.Alipoingia katika ubunge ilikuwa wazi kuwa Kubenea alikuwa na hasira na hii ilionekana dhahiri katika matamshi yake.
Hivyo hivyo Lema.Kapitia taabu nyingi katika kuondoa chama tawala katika mji wa Arusha.Mengi yamefanyika ya kumkwamisha na hata wakati mwingine wapanga mbinu kushindwa kutofautisha kumuumiza Lema na kuumiza wananchi.
Ushauri wangu kwa Lema ni kuwa hii ni awamu yake ya pili ndanii ya bunge na kama alivyokiri kuwa ni mtu wa maombi na kufunga basi aachane na siasa za bei chini amuige mbunge wa Bukoba ambaye alipata mateso kwa kusingiziwa na waliotoa viapo vya ushahidi leo wanakula pepo hapa duniani.
Hebu Lema rudi katika kujenga hoja ndani ya Bunge,Muache JPM na Mungu wake.
Clips zinasambaaa toka ndani ya bunge zina ujumbe muhimu kwa upinzani.Wenzenu wanafanya pre-emptying measures na wana win confidence ya Wananchi.
Kwa Polisi hebu jaribuni kupima na kutumia weledi wenu lakini pia tuna idara yetu ya Usalama ambayo ina uwezo wa kujua tishio la Lema kwa Taifa.Kama tishio ni kubwa basi apumzishwe mahali ili amani na utulivu viendelee.
 
Huyu naye achunguzwe jee hana kitambulisha kama kile?
UNDERCOVER AGENT
SPECIAL FORCE
 
Kukosa busara na ustaarabu ni moja wapo ya sifa kuu ukawa!
 
POLISI ARUSHA WALIMTAKA JESHI LA LEMA LIMKAMATE UVCCM.
msiniulize maswali, napenda ujinga wenye faida.😱
Geshi rimeitikia wito wa UVCCM na sasa wamemkamata Lema.

Hongera CCM kwa kuiamrisha polisi
 
Back
Top Bottom