UVCCM Arusha gumzo

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
IMG-20170501-WA0010.jpg

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Vyuo na Vyuo Vikuu katika Mkoa wa Arusha tumekuwa na Katibu NEC Itikadi na Uenezi ndugu Humphrey Polepole ambaye amekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Vijana wa CCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha .

Katika hatua nyingine ndugu Humphrey Polepole ametoa Vyeti kwa Wahitimu 268 na kupokea Wanachama Wapya wa CCM zaidi ya 65 na Kuwapa Kadi za Uanachama na kisha kuwaongoza kiapo cha uaminifu ndani ya CCM. Mahafali yaliyoudhuriwa na Wanachama 523.

"Naomba nipatiwe taarifa zao wahitimu wote pamoja na majina yao kwa ajili ya matumizi zaidi" watatusaidia katika ujenzi wa Taifa. Kauli hiyo imekuwa GUMZO.

[HASHTAG]#Modern[/HASHTAG] UVCCM#
[HASHTAG]#CCM[/HASHTAG] MPYA ,TANZANIA MPYA#
 
Ikija zamu ya mahafari ya wanafunzi wa vyama vya upinzani nao wapatiwe nafasi kama hii.
 
aibu majitu yaliyoelimika yapo na kungangania ccm so shame!
pamoja na elimu yako ukawe ccm?
The bululaz vilaza hao
Wachumia tumbo
 
Hivi wewe ndio DC uliyeteuliwa kuleta viwanda ! Polepole huyu huyu mchumia tumbo anayeamini katika serikali 3 ndiye unatuletea hapa ?
 
Hizi buku 7 saba hizi zinawasumbua sana hao vijana...

Wasomi bado ni watumwa kwa wanasiasa
 
View attachment 503455
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Vyuo na Vyuo Vikuu katika Mkoa wa Arusha tumekuwa na Katibu NEC Itikadi na Uenezi ndugu Humphrey Polepole ambaye amekuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Vijana wa CCM Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha .

Katika hatua nyingine ndugu Humphrey Polepole ametoa Vyeti kwa Wahitimu 268 na kupokea Wanachama Wapya wa CCM zaidi ya 65 na Kuwapa Kadi za Uanachama na kisha kuwaongoza kiapo cha uaminifu ndani ya CCM. Mahafali yaliyoudhuriwa na Wanachama 523.

"Naomba nipatiwe taarifa zao wahitimu wote pamoja na majina yao kwa ajili ya matumizi zaidi" watatusaidia katika ujenzi wa Taifa. Kauli hiyo imekuwa GUMZO.

[HASHTAG]#Modern[/HASHTAG] UVCCM#
[HASHTAG]#CCM[/HASHTAG] MPYA ,TANZANIA MPYA#
POLEPOLE BADO KABISA KWA MOSESS NNAUYE ANALAZIMISHA TU...
 
Unakuja kwenye MAHAFALI CHA VYUO unaongea na UVCCM halafu unasema UVCCM wa mkoa wa Arusha? hao wote walikuja kupata elimu waliosalia kuwa ni wa Arusha ni wachache sana, ukihitaji UVCCM Arusha nenda pale mtaa wa pangani utawakuta wanakula mirungi tu na hawaguswi kwa kuwa ni chama tawala, yaani wale wanafaa kwa matumizi ya kurusha mawe tu na mipasho. kama anatafuta warusha mikuki wa olimpic na waimbaji TOT taarabu amepata.
 
Back
Top Bottom