UVCCM Arumeru hawaeleweki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM Arumeru hawaeleweki

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Feb 25, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jimbo la Arumeru Mashariki umeomba Kamati ya Utekelezaji ya Wilaya na Mkoa ya Vijana kumchukuliwa hatua za kisheria Kennedy Mpumilwa kwa madai ya tabia ya kuharibu umoja huo.

  "Huyu ni wakala wa Chadema kwani amekuwa akijichukulia madaraka yasiyo yake na tunamwomba asionekane kuvaa sare za CCM wala kushiriki kamapeni za CCM .

  Waliongeza kuwa hivi sasa vijana wa jimbo hilo wanasubiri vikao vya juu vimalize uteuzi wake na kurudisha jina la Sioi Sumari, walisikia wakisema endapo jina la Sioi litakatwa na kumrudisha mgombea wasiyemtaka, nao wataamua nani wamchague.

  My Take: Kama wanamtaka mwenzao (Mpumilwa) afuate demokrasia kwanini basi na wao wanatishia kutokubaliana na vikao vyao vya juu endapo jina la Sioi halitarudishwa?

  Gazeti la HabariLeo.
   
 2. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #2
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huu ni uzushi mtupu. Uvccm Armeeru wako tayari kutetea mgombea yeyote atakaeteuliwa na kamati kuu. Hawani mkataba na mtu yeyote mbali na ccm ambacho ndiyo chama chao.. Inaonekana cdm ndiyo mnamhitaji Sioi ili iwe rahisi kumshinda. Tafiteni mgombea wenu wa ccm iachieni ccm.
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mzee habari hii imetoka gazeti la HabariLeo si uzushi labda kama habarileo nao wameanza kuizushia CCM

  UVCCM wavurugana Arumeru

  UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM) Jimbo la Arumeru Mashariki umeomba Kamati ya Utekelezaji ya Wilaya na Mkoa ya Vijana kumchukuliwa hatua za kisheria Kennedy Mpumilwa kwa madai ya tabia ya kuharibu umoja huo.

  Pia umemtaka kutovaa sare za CCM wala kushiriki kampeni zozote za chama hicho wakati wa kuelekea uchaguzi mdogo wa Jimbo hilo Aprili mosi.

  Wakizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi ya CCM Kata ya Kikatiti mkoani hapa, Mwenyekiti wa Arumeru Mashariki, Ombeni Pallangyo, alisema Mpumilwa hivi karibuni alitoa tuhuma kwenye gazeti moja kuwa ni mjumbe wa Baraza la Vijana Mkoa.

  Alisema Mpumilwa alidai CCM Arumeru imeanza kuvurugana na kuongeza kuwa taarifa hiyo ni ya uongo na hakitakii chama hicho mema bali ni mvurugaji ambaye ni mjenga hoja za kubomoa na kuharibu UVCCM Arumeru.

  Pallangyo alikwenda mbali kwa kusema kuwa Mpumilwa ambaye anajitambulisha kama Mjumbe wa Baraza la Vijana Mkoa ni wakala wa Chama cha Upinzani na ndio maana imefika mahali akaandika waraka wa uongo kudai kuwa CCM Arumeru wanaanza kuvurugana.

  Aliongeza kuwa hivi sasa vijana kutoka kata 17 za jimbo hilo wanasubiri vikao vya juu vimalize uteuzi wake na kurudisha jina la Siyoi Sumari ambaye alichaguliwa kwa kura 361.

  "Huyu ni wakala wa Chadema kwani amekuwa akijichukulia madaraka yasiyo yake na tunamwomba asionekane kuvaa sare za CCM wala kushiriki kmapeni za CCM wakati huu ambapo vijana wa CCM tutakuwa tupo kazini tukinadi sera za chama chetu kulekea uchaguzi mdogo wa Jimbo, Aprili mosi."

  Alisema msemaji wa UVCCM wilayani Arumeru ni Mwenyekiti, Katibu au pale inapobidi mhamasishaji kwa niaba ya Umoja wa Vijana na si Mpumilwa ambaye hana nafasiya uongozi kwenye umoja huo na kuongeza kuwa wapo wenyeviti wa kata ambao kila mmoja kwenye kata yake anafanya kazi kwa mujibu wa kanuni za umoja huo.

  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James ole Millya, alisema kwenye harusi huenda waalikwa na wazamiaji hivyo jimbo hilo ni la CCM na kuwasihi vijana kuhakikisha wananadi sera za chama hicho na mwisho wa siku kuchukua jimbo hilo.

  Mpumilwa alipopigiwa simu na mwandishi wa habari hizi kuzungumzia tuhuma dhidi yake alipokea na kudai kuwa yeye hawezi kuzungumza juu ya tuhuma hizo na kusisitiza kuwa hana cha kusema."Ndugu mwandishi no comment (sina cha kusema)".

  Hata hivyo, vijana hao awali kabla ya tamko hilo walisikia wakisema endapo jina la Siyoi litakatwa na kumrudisha mgombea wasiyemtaka, nao wataamua nani wamchague, lakini walisisitiza kuwa wanachosubiri ni jina la Siyoi kurudishwa kwao kwani ndiye aliyepitishwa na wajumbe Februari 20. Siyoi alipata kura (361), Rishiriankira Urio (11), Elishilia Kaaya (176) , Elirehema Kaaya (205) William Sarakikya (259) na Anthony Musani (22).

  Baada ya UVCCM kutoa tamko hilo baadhi ya wazee wa kabila la Wameru "Washiri" eneo la Kikatiti waliwambia waandishi wa habari kuwa hawajawahi kutoa tamko la kumkataza Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kushiriki kampeni kwenye jimbo hilo.

  Wazee hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao walisema kama tamko hilo lipo, basi lilitolewa na baadhi ya wazee wa kabila hilo, lakini wengine hawalijui, kwani hawajawahi kumjadili Lema kwenye vikao vya wazee kuwa asikanyage hapo na kuongeza kuwa habari hizo walizisikia magazetini na ni propaganda.

  Waliongeza kuwa hawajamzuia Lema wala Chadema kufika eneo hilo la Meru na kuongeza kuwa Arumeru ni jimbo lenye amani, hivyo walimkaribisha Lema na chama chake kushiriki kampeni na mwisho wa siku wananchi ndio watatoa jibu sahihi ya nani apite kuongoza jimbo hilo ambalo lina changamoto zinazohitaji ufumbuzi.
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Feb 25, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Arusha mjini tuliomba sana CCM wamsimamishe Batilda, ombi letu likapata kibali machoni pa Bwana wa Majeshi, hivi sasa tunajivunia kamanda Lema. Arumeru tunaomba sana CCM wamsimamishe Sioi ili mwishowe tujivunie kamanda Nassari
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Feb 25, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Kenedy ana wenge sana , tokea sekondary alikuwa hivyo . Nimeshangaa kusikia ni kiongozi uvccm sana . Au sijui ni kwa sababu baba yake danford mpumilwa ana jina arusha.
   
 6. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #6
  Feb 25, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nani kakuambia kenn ni mtoto wa Danford?ishu ni kwamba Mkiti wa UV-CCM mkoa wa Arusha Millya ndiye anayewakorofa wenzake kwa maelekezo ya EL ambaye ni mkwe wa Sioi wanashinikiza jina lake lipitishwe na vikao vya chama na viongozi wa wilaya hawamtaka coz CDM wanaweza kushinda kwa urahisi uchaguzi huo kwani Sioi hauuziki Arumeru!
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Endelea kushangaa hivyo hivyo mwenzako anapopanda ngazi.
   
Loading...