Uvamizi ndani Mgodi wa Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvamizi ndani Mgodi wa Geita

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TaiJike, Apr 5, 2012.

 1. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Kuna rafiki yangu mmoja kanipigia simu na kusema kuwa mgodi wa Geita umevamiwa na watu wanaoiba mawe yenye dhahabu maarufu kama magwangala, wamefunga baadhi ya barabara za ndani ya mgodi kwa kupanga mawe makubwa ili kuzuia magari madogo na mabasi yanayopeleka wafanyakazi mgodini humo. Nitawaletea taarifa zaidi kadri ntakavyozipokea.
   
 2. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Askari wa mgodi wamefanikiwa kuwaondoa wavamizi hao ingawa kuna uharibifu ktk magari mawili yamevunjwa vioo, na hali yaonekana kuwa shwari kwa sasa mgodini, ila imekuwa ni khofu kwenye kijiji cha nyamalebo kilicho jirani na mgodi, kwani wavamizi hao wamekimbilia huko.
   
 3. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Taarifa niliyonayo, Gari mbili mgodini zachomwa moto, hakuna madhara kwa binadamu mpaka sasa.
   
 4. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hii hali inaleta wasiwasi jamani, hasa kwa sisi ambao tuna kaka zetu huko :(
   
 5. bulinge

  bulinge Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali sio shwari kwanini magari ya mgodini hayatakiwi kupita barabarani za mjini na muda mfupi polisi wamefanikiwa kuwasambaza watu waliokuwa wamekusanyika jilani na kituo cha polisi cha Geita.
  Pia gari moja ya GGM iliyokuwa inatokea barabara ya katolo imeshambuliwa na wachimbaji wadogo.
   
 6. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ni kweli mwali hali si shwari mpaka sasa geita mjini, gari za mgodi zimezuiwa kutoka nje ya mgodi.
   
Loading...