Uuzaji nyaya za cable wapigwa marufuku

Uuzaji nyaya za cable wapigwa marufuku

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marukufu kuuzwa kwa nyaya za kupitia mawasiliano (Data Cable) zilizokuwa zikiuzwa kwenye baadhi ya maduka ya vifaa vya kielektroniki baada ya kubainika hazikidhi viwango.

Hatua hiyo ilifikiwa na maofisa wa shirika hilo kwenye baadhi ya maduka jijini Dar es Salaam baada ya sampuli za nyaya hizo kupimwa kwenye maabara na kudhibitika hazikidhi viwango.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkaguzi wa TBS, Saimon Emmanuel, amesema tayari wenye maduka yaliyokuwa yakiuza nyaya hizo wamepewa muda wa siku 14 kujieleza .

Pia amesema baada ya kupimwa kwenye maabara za shirika pamoja na kasoro nyingine, nyaya hizo zilibainika kuwa na kiwango kidogo cha madini ya shaba (copper) na kwamba hata nguvu kinzani kwenye nyaya hizo zilifeli kwenye maabara .

"Hivyo tumezizuia kwenye maduka tukisubiri hatua nyingine," amesema na kutoa mwito kwa wafanyabiashara wanapotaka kununua bidhaa kutoka nje ya nchi kuhakikisha zinakaguliwa ubora wake nje ya nchi kabla hazijaingia nchini mpangao ambao kitaalamu unaojulikana kama kama Pre-Shipment/Export Verification of Conformity to Standards (PVoC).

Pia ameongeza kuws wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi bila kukabuliwa kupitia PVoC, pindi bidhaa zao zinapofika nchini wanatozwa faini ya asilimia 15 kulingana na thamani ya mzigo, kulipia gharama za upimaji kwenye maabara na kwamba zinapofeli kufikia viwango muagizaji anaamuriwa kuzirudisha alikozitoa kwa gharama zake au kuteketezwa hapa nchini pia kwa gharama zake.

Emmanuel amesema hiyo ni kwa mujibu wa Sheria Na:2 ya Viwango ya mwaka 2009. Ametoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wazingatia sheria na taratibu ili kuepuka hasara.

Shirika hilo kwa sasa linaendesha awamu ya pili ya msako wa kushtukiza wa bidhaa zilizopo sokoni ili kubaini bidhaa ambazo hazina ubora na kuziondoa kwenye soko
 
Ziliingiaje?
 
Hapo naunga mkono hoja ilifika hatua mpk mtu unatafuta cable za mtumba bwana kutafuta ubora msiishie datacable pekee za computer na simu pekee zingine pitieni na za video cable za Dvd na audio to subwoofer au tv wanazipaka rangi ya kopa wakat ni aluminium pia powercable za umeme zilizochini ya viwango zipigwe marufuku kabisa 7bu zinatia hasara na hatari kwa usalama wasojua wanaharibu vifaa vyao bila kujua kwa hilo nawapongeza

Sent using data cable
 
[emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106][emoji106]
Hapo naunga mkono hoja ilifika hatua mpk mtu unatafuta cable za mtumba bwana kutafuta ubora msiishie datacable pekee pitieni na cable za computer au simu pekee zingine za video cable za Dvd na audio to subwoofer au tv wanazipaka rangi ya kopa wakat ni aluminium pia powercable za umeme zilizochini ya viwango zipigwe marufuku kabisa 7bu zinatia hasara na hatari kwa usalama wasojua wanaharibu vifaa vyao bila kujua kwa hilo nawapongeza

Sent using Jamii Forums mobile app

Siyakukothamela Sonini na nini
 
Hivi hili Shirika la Umma si Wana kitengo Chao kwenye kila port of entry?..The level of incompetence of these guys is from out of this world.
 
Isije ikawa janjajanja zao ili mladi wapate pesa

Love and peace
 
Tatizo linaletwa na watengenezaji wenyewe na baadhi ya watu..
Kwa mfano kuna watengenezaji wanatoka nazo nje kwao zinapelekwa tbs kupimwa zikishapitishwa kuwa zinafaa tayari kuna wawekezaji hapa rafiku au ndugu wa watengenezaji wanazifyatulia hapa hapa haraka haraka wanaziingiza sokoni na kibali wanatumia kile kile walichoruhusiwa nacho na tbs..
Shida ni kuwa tbs hawako clear na baadhi ya viwanda vilivyoanzishwa hapa tz ..
Wakati mwingine unakuta kiwanda kina ushajili wa kutengeneza mafuta ya kula..
Lakini humo humo mdani usiku wanafyatua sabuni au pipi au biskuits..
Ziliingiaje?
 
Sio njia ya panya tatizo wanaleta zinapelekwa tbs wakishapewa kibali cha kuziingiza hapa nchini kuna wenzao wanazifyatulia hapa hapa tz . Kuna magordawn kibao nje yameandikwa ndani wanashughulika na nn lakini humo mdani usiku wanatengeneza kitu kingine
bila Shaka njia za panya Labda
 
haya mambo yawe endelevu, tena kuna cable nyingi sana za ajabuajabu madukani kazi bado ni kubwa.
 
Wewe na TBS mnaugua wazimu. Wewe unaandika uuzaji wa nyaya za cable umepigwa marufuku, wakati si kweli, zilizopigwa marufuku ni ambazo hazikidhi viwango.
TBS wanaruhusu nyaya feki zinaingia nchini, au wanaruhusu nyaya za chini ya kiwango kuzalishwa viwandani halafu wanaenda kuwakamata wenye maduka, kwani wao ndio wamezalisha?
 
Sio njia ya panya tatizo wanaleta zinapelekwa tbs wakishapewa kibali cha kuziingiza hapa nchini kuna wenzao wanazifyatulia hapa hapa tz . Kuna magordawn kibao nje yameandikwa ndani wanashughulika na nn lakini humo mdani usiku wanatengeneza kitu kingine
Kumbee Dah sio mchezooo
 
Kiwanda/kampuninhusika ndio iwajibishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo linaletwa na watengenezaji wenyewe na baadhi ya watu..
Kwa mfano kuna watengenezaji wanatoka nazo nje kwao zinapelekwa tbs kupimwa zikishapitishwa kuwa zinafaa tayari kuna wawekezaji hapa rafiku au ndugu wa watengenezaji wanazifyatulia hapa hapa haraka haraka wanaziingiza sokoni na kibali wanatumia kile kile walichoruhusiwa nacho na tbs..
Shida ni kuwa tbs hawako clear na baadhi ya viwanda vilivyoanzishwa hapa tz ..
Wakati mwingine unakuta kiwanda kina ushajili wa kutengeneza mafuta ya kula..
Lakini humo humo mdani usiku wanafyatua sabuni au pipi au biskuits..
Matango pori humu ni mengi sana.
Watanzania na ujanja wetu bado hatujawa na uwezo wa kutengeneza hata hizo nyaya feki.
Naomba tufanye utafiti kabla hatujasema
 
Back
Top Bottom