Uuaji katika jami

Uuaji katika jami

XhosaVica

Senior Member
Joined
Sep 29, 2020
Posts
157
Reaction score
155
Kutumia risasi za moto kutuliza vurugu si sawa. Hasa kwa chombo ambacho wananchi wanadhani kimeundwa kuwalinda na kuwaonyesha njia ya amani.
Hakika damu haiendi bure, roho zinazotolewa kabla ya muda wake zitaililia nchi na nchi haitakuwa sehemu salama. Ni vyema weledi na hekima ikatumika katika kutatua matatizo ya jamii. Tulio hai tusiposema na kutenda matukio yatasema. Tabia nchi itasema, mapigo juu ya nchi yatasema. Inahumiza kupoteza rafiki, mwenza, jamaa, mtoto. Na inakwaza zaidi kumpoteza kwa kuipigwa risasi.
Tumepoteza ndugu kwa ajali ambazo zingezuilika kwa kuwa na miundo mbinu bora( barabara na magari) na umakini wa madereva.
Tumepoteza watu kwa kuwa na elimu hafifu, utayari na kujali juu ya huduma ya afya.
Umeme, maji imekuwa ni kitu cha anasa katika nchi ya Tanzania ambayo ina vyanzo vingi vya maji mito na maziwa.
Uongozi umekuwa ombwe. Watu bora hawaendi kugombea kisa ya woga na dhana mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusema siasa ni mbaya. Wananchi wengi hawafanyi takwa lao la msingi la kujiandikisha, kupiga na kulinda kura sababu kuu ikiwa ni woga. Unawezaje kuogopa mtu ambaye siku zake hapa duniani zinahesabika.? Na ilihali usipotimiza wajibu wako inaathiri nchi na uzazi wako.?
Inafikirisha mno. Wakati ni sasa kutenda iliyo sawa.
Namaliza kwa kusema damu za wahanga wanaouwawa zitawalilia wauaji na vizazi wao na hakika Amani haitakaa itokee mioyoni mwao.
 
Mwandiko mbaya unaumiza macho ukisoma sijamaliza kusoma kichwa kimeuma
 
Muda wa reformation umefika lazima Kuna maumivu mengi sana!

Tuombe mungu 2027 itukute TU wazima maana mti wa kijani utapukutisha majani kabla,wakati na baada ya uchaguzi!

Kijani imekosa Baba mwadilifu wa kukemea uhuni na ubadhirifu kama Mzee mkapa,kikwete Ni Mzee kijana hata Mimi siwezi mwelewa kabisa,mwinyi ameshaenda,wamebaki Mzee Pinda,Chiligati,Mkuchika ndio nawaona wanaweza walau kukemea uhuni!!

Kazi tunayo sana!
 
Back
Top Bottom