Uturuki yapata pigo kubwa vitani Syria

Uturuki yapata pigo kubwa vitani Syria

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
_99878924_f150ee16-f231-44e1-876e-5cdc47c58b52.jpg

Jeshi la Uturuki, limepata pigo baya mno vitani, katika makabiliano yake dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi ndani ya Syria Kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya wanajeshi wake 7 kuuwauwa.

Wanajeshi watano waliuwawa, baada ya kifaru chao kushambuliwa katika eneo la Afrin

Waziri mkuu Binali Yildirim, ameapa kuwa wanamgambo hao "watalipia uovu wao maradufu".

Mara tu baada ya matamshi hayo kutoka Ankara, ndege za kijeshi ziliangusha mizinga mizito mizito kulenga ngome za Wakurdi Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.

Operesheni ya Uturuki iitwayo "Olive Branch" ilizinduliwa Januari 20, ili kuwafurusha wanamgambo wa kikurdi wa YPG kutoka maeneo ya Afrin.

Katika taarifa kutoka idara ya jeshi la Uturuki, wapiganaji wa YPG walishambulia kwa makombora kifaru moja ya jeshi lake katika eneo la Sheikh Haruz, Kaskazini Mashariki mwa mji wa Afrin.

Chanzo: BBC Swahili
 
Jeshi la Uturuki, limepata pigo baya mno vitani, katika makabiliano yake dhidi ya wanamgambo wa Kikurdi ndani ya Syria Kaskazini mwa nchi hiyo, baada ya wanajeshi wake 7 kuuwauwa.

Mkuu, askari 7 kuuwawa hilo ni pigo kubwa? Kama ni pigo kubwa ukiangalia jumla ya askari wetu waliokufa DRC itakuwa nini kwetu? Ni vita gani ambayo unaenda kupigana ukitegemea hutapoteza askari hata mmoja?
 
Na

Mm nmewaza hvyo..
 
Nimeona sehem kwamba ndege ya russia imetunguliwa huko idibl Syria sijui nitukio la leo?.
 
Kwa sababu siyo weusi ndo maana ni pigo kubwa. Wakwetu 14 na hukusema tumepata pigo kubwa sana.
 
Back
Top Bottom