Babu sea angalau nimeona kwako kitu!
Wakati ule Uturuki anapata ujasiri wa kuangusha ndege ya Urusi alikuwa na mawazo mawili labda mbadala.
Kwanza aliwaza kuwa 'ahh! Niko kwenye mchirizi wa mafuta bwana, mimi ndio mtu wa kati kutoka syria na Iraq, biashara ni nzuri na nnaweza tengeneza pesa nyingi'
wakati huo alikuwa hajui siri ya biashara ya mafuta iko kwa muuzaji, muuzaji hasemi kirahisi na hivyo sio rahisi kupata picha ya soko.
Sasa leo kuna uzalishaji uliozidi mahitaji, uzalishaji unaosababisha mzigo usiokubalika refineries kubaki ndani ya meli ukielea juu ya maji. Huu ni mtaji, huu ni uwekezaji usioleta tija inayokubalika kwa sasa, hili ni tatizo.
Wazo la pili lilikuwa kuegemea Jumuiya ya Ulaya kama partner mpya mwenye nguvu inayoongezeka. Mwenye uwezo, watu wengi, nia ya kukua n.k
juhudi za Erdogan kujiunga na jumuiya hii kwa miaka 16 sasa zinaeleza kila kitu. Hapa napo Bundi akatua, UK ikajitoa na ramani ikashindwa kusomeka.
Huku uhusiano wake na ISIS unazidi kutokutabirika.
Hapa dawa ni kurudi kwa zimwi likujualo, marafiki wa zamani, Russia na Israel.