Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,114
- 34,956
Ilionekana kama jambo la kijinga, jamaa mmoja alikuwa anamsifu mtoto wake kuwa anaakili sana kwa sababu anaharibu sana vitu vya nyumbani.
"Yani", alisema huyo jamaa; "haipiti siku mbili lazima atatia hasara, kama sio kuvunja vyombo basi ataharibu simu au 'rimoti'".
Mmoja kati ya jamaa tuliokuwa tukimsikiliza akaauliza; "sasa hiyo akili au ujinga? Watoto wa aina hiyo ni wajinga, usisema wana akili", akasema.
Ilivyoonekana ni kwamba watu wengi walimuunga mkono huyu jamaa wa pili aliyesema kuwa anachofanya mtoto wa jamaa wa kwanza ni ujinga na si akili, lakini mwenye mtoto 'mwenye akili' hakukubaliana nao, alisisitiza kwa sababu nyepesi nyepesi kuwa mtoto wake ana akili.
"Mtoto asiyekuwa na akili hawezi kushika rimoti, atashika aifanyie nini?" alisema baba wa mtoto 'mwenye akili'.
Kufikia hapo, nikashawishika kumuuliza kuwa mtoto wake ana umri gani, akasema; "ana miaka minne sasa".
Sikupenda kuwa na jibu lakwangu binafsi juu ya mtoto wa umri huu mwenye tabia ya kuvunja vitu, akili ikanituma kutauta hisia za watu wengine wanamchukulia vipi mtoto wa aina hii.
"Watoto wa aina hiyo ni manunda", anasema Emmanuel Mkumbo, mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam.
Tafsiri yake kwa neno 'nunda' anaitoa kwa kusema; "hao ni watoto waharibifu na wanaonyesha tabia yao tangu utoto, kwa hiyo mzazi anatakiwa kuwa macho nao sana, ukiwalegezea watakutia hasara".
Mkumbo anaongeza; "kwa umri huo mtoto anatakiwa awe mtulivu, ni mtu wa kuongozwa na wazazi wake, sasa akiianza umapepe ndio hukawii kusikia ameungua na moto au amenasa kwenye umeme".
Kwa ushauri wa Mkumbo, wazazi wenye watoto wa aina hii hawapaswi kuona fahari bali wanapaswa kuwa na tahadhari na ikiwezekana kuanza wawe wakali ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea mbeleni.
Tofauti na mtazamo wa Mkumbo, Idrisa Kavishe, mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam yeye anawachukulia watoto wa aina hiyo kivingine kabisa, anasema:
"Kwa umri huo huwezi kusema ni mtoto mjinga, mtoto wa umri huu huwa hajui kitu ila anajifunza, kwa kawaida wanaitwa watoto watundu".
Kwa mtazamo wake, Kavishe anasema; "mtoto anapokuwa mtundu anaelekea katika kujifunza matumizi ya vitu vinavyomzunguka, anapenda kuvishika na kuvitumia kama watu wakubwa wanavyotumia, huu ndio utundu wenyewe".
Ikiwa tunakubaliana na Kavishe, kuwa tafsiri ya watoto wenye kuchezea au kuvunja vitu ni watundu, wenye tamaa ya kujifunza, hukumu yao katika hilo itakuwa ni wadadisi, na kwa umri walionao udadisi wao unawaza kutafsiriwa kama akili.
Kwamba wanachofanya watoto wa aina hii ni kujifunza matumizi ya vitu vinavyowazunguka katika mazingira yao, kwa hali hiyo uishughulisha akili yao na kwa hilo wanaweza kuingia kwenye fungu la 'wenye akili'.
Inawezeka kuwa Kavishe na Mkumbo wote wako sahihi, lakini saikolojia ya watoto inawatafsiri vipi watoto wa aina hii?
"Ni watoto wenye akili", anasema Denis Munga mtaalamu wa masuala ya saikolojia ya watoto.
Kama alivyofikiri Kavishe, Munga anasema; "ili kufahamu kama akili za mtoto zinafanyakazi viziru kwa umri huo wa miaka minne, mzazi anatakiwa achunguze kama mtoto ana tabia ya kushughulishwa na vitu vilivyo karibu yake.
"Kwa mfano, unaweza kumwekea mtoto mpira (wa kuchezea) karibu yake, kwa akili za haraka hapa unatarajia kuwa atauchukua na kuanza kuchezea, kinyume cha hapo unaweza kuingiwa na mashaka kuwa labda hajauona au haupendi.
"Kwa kufanya hivyo, unaanza kugundua kuwa mwanao hayuko sawa, kwa sababu hajafanya tendo la kawaida kwa akili za watoto wa umri wake, akiuchukua, pengine inaweza isikushughulishe tena kumchunguza kwa sababu atakuwa amefanya jambo la kawaida kwa akili za watoto."
Kwa mtiririko wa aina hii ya matukio, uwezo wa kufanyakazi kwa kawaida kwa akili ya mtoto huanza kupimwa hapo na wazazi wanashauriwa kuwa wachunguzi wa tabia za watoto wao hasa kwa umri huo, miaka mitatu kuendelea hadi mitano na wakati mwingine hadi sita.
Munga anasema; "hata hivyo wazazi wanapaswa pia kuwa waangalifu sana kwa watoto katika umri huo, wakishafahamu kuwa watoto wao ni watundu, ambacho ndicho kipimo cha akili, wanapaswa kuwawekea mazingiri ambayo utundu wao hautoweza kuwazuru".
Mazingira hayo ni pamoja na kuwaweka mbali au kuviweka mbali vitu vinavyoweza kuwadhuru ikiwa ni pamoja na dawa.
"Pia wazazi wasiwe na tabia za kuwafokea wanapoleta uharibifu", anasema Munga nakuongeza; "bali wawaondoe kwa upole kwa sababu kuwafokea kunaweza kuharibu ile akili yao ya udadisi na kuanza kujenga woga ambao utawafanya kuharibu uwezo wao wa kiakili".
Inawezekana ukawa na mtoto wako mdogo, ni mtundu na anavunja sana vitu nyumbani, kwa hilo unapaswa ujivunie na ujaribu pia kumnunulia vitu vingi vya kuchezea ili asitiea hasara, na kuwa na fahari naye kwa sababu anaonyesha kuwa ana akili!