Ndugu mwana jamii forum soma kipande hiki toka gazetini
Kihusucho utumwa hiari.
Je tufanyeje nini kwa vijana wetu ili waepuke aina hii ya utumwa?
From RAIA MWEMA 18/02/2009
UTUMWA WA HIARI WAJA
Sasa tujiandae kushuhudia watoto wetu wakikimbilia utumwani kwa maelfu,
Wazazi na ndugu wa karibu wa vijana wa Afrika wanatakiwa wajiweke tayari kisaikolojia kukabiliana na upotevu wa vijana wao watakao ondoka hivi punde kujipeleka katika utumwa wa hiyari.
Wanakwenda wapi? Ni kulekule Marekani ambako walipelekwa mamilioni ya waafrika walio uzwa huko kama Punda wabeba mizigo. Wa afrika ndiyo walio jenga ukwasi mkubwa wa Wamarekani.
Rais wa sasa ambaye ni mweusi anataka watu wengi wa kujitolea hasa Weusi kwenda kumsaidia kupigana katika vita ambazo vijana wa Marekani wanazikacha, Kama hii ya Afghanistan.
Marekani wanasema kijana yeyote asiye kuwa raia wa Marekani anayetaka kuwa Raia atapewa uraia ndani ya miezi sita tu alimradi awetayari kujiunga na majeshi ya Marekani kwenda kupigana Afghanistan na kwingineko.
Utaratibu huu ulifanyika wakati wa vita vya Vietnam ambavyo kwa ukali wake ilihitaji vijana kutoka mataifa Mengi Duniani hasa kutoka dunia ya tatu na wakahongwa biskuti ya URAIA.
Habari hizi bila shaka zitakuwa na ladha ya bongo Flava kwa vijana wetu wana pita wa kisema Bora Mbwa Ulaya kuliko Mswazi Bongo Watahamia Marekani tena kwa wingi siyo tu kwa sababu wameitwa kwenda huko bali pia kwa sababu Nchi hii haielekei kujua nini inataka kufanya na vijana wake.
Wameachwa wanamea kama magugu katika mahame. Hawajajengewa matumaini katika maisha yao ya badaye.na ni kweli kwamba wanaweza kuamini kwamba ni bora kuwa mtumwa Ulaya kuliko kuwa huru Afrika