figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Heshima kwenu wakuu,
Napongeza Mpango wa Serikali ya Tanzania wa kuhamia Dodoma kwani zimekuwa stori za muda mrefu. Ila hili swala la kuhama ili kumfurahisha rais tuliangalie mara mbili.
Jana wakati tunahama, nlijua tunaenda sehemu iliyoandaliwa kumbe bado ujenzi unaendelea, nahisi lengo ilikuwa ni kuwa wa pili kuhama baada ya Waziri mkuu. “Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba 2016,Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza azma hii ya serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa watanzania kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka kwenda Dodoma”,Alisema Mhe. Kairuki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye makao makuu ya nchi.
Baada ya kufika Dodoma nikashangaa kukuta Ujenzi unaendelea na mbao mbao za mafundi bado zipo ndani ya Nyumba na mafundi wakiendelea na Ujenzi. Swali najiuliza, je tulihama ili kumfurahisha rais au tulihama kwa mashindano sababu waziri Mkuu kahama?
Makao makuu ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mkoani Dodoma ambayo ndo wamehamia, ikiwa bado kwenye Ujenzi(Kwa ufadhiri wa UDOM).
Hii ya kufanyia kazi kwenye Jengo/Nyumba ambayo bado ujenzi unaendelea mnaichukuliaje kiusalama kwa Wafanyakazi? Hii ni Hatari sana, nahisi hapa kuna sheria ya Usalama imevunjwa.
Karibuni kwa Mjadala.