Taarifa kwa Umma kusuhu Tangazo la kazi la tarehe 26 Machi, 2013. Waombaji wa nafasi za kazi Serikalini kwa tangazo lililokuwa limetolewa tarehe 26 Machi, 2013 kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ambalo mwisho wa kutuma maombi ilikuwa terehe 9 Aprili, 2013 wametakiwa kuangalia majina yao katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuanzia tarehe 13 Mei mwaka huu ili kujua endapo wamechaguliwakwa ajili ya kufanya usaili wa nafasi walizoomba.