Utumiaji wa dawa asili za mizizi, je unaathari yoyote kiafya?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utumiaji wa dawa asili za mizizi, je unaathari yoyote kiafya??

Discussion in 'JF Doctor' started by Uncle Jei Jei, May 6, 2012.

 1. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  Nimepata kusikia kuwa mizizi yoyote itumikayo kama dawa, pamoja na kutibu ugonjwa husika, pia huimarisha misuli (dauble advantage), je kuna ukweli wowote?? Na kama zinafaida, kwanini watu wengi hubeza dawa za kimasai ambazo asilimia kubwa ni mizizi?? Pia kama zina madhara, ni yapi hayo?? Nawasilisha kwa wataalam, naamin humu wapo madokta waliosomea vitu mbalimbali, naomba kufahamu kwani kuna tatizo linanisibu na wengi wananielekeza mizizi, naogopa isijekuwa inaondoa tatizo kwa mda,then linajirudia kama mwanzo. Daima JamiiForum imekuwa msaada kwa jamii!
   
 2. Fadhili Paulo

  Fadhili Paulo Verified User

  #2
  May 6, 2012
  Joined: Sep 1, 2011
  Messages: 3,241
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 135
  Ni tatizo gani hilo linalokusibu? si ungesema tu pengine ungehitaji mazoezi tu, anyway usihofu mzizimkavu atakuja siyo muda, subiri hapo hapo katika bench kaenda kunywa maji.
   
 3. M

  Moony JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tafuta kitabu au google neno " PHARMACOGNOSY" utaelewa vizuri zaidi.

  Mimea mingi tuseme mimea ina therapeutic effects katika aidha magome, majani ama mizizi. Hi inakuwa na alkaloids ama glycosides ambazo kutegemea na content ya dawa iliyomo inaweza kuwa na madhara au siyo na yakatibu ama kuharibu katika concentration fulani.
   
 4. F

  Fofader JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Mkuu kuna tawi la kemia linaitwa phytochemistry na uzoefu unaonyesha kwenye miti iwe mzizi, stem au majani kuna aina mbalimbali za chemical compounds kufikia hata mamia!! Kwenye mti mmoja na kwa wingi tofauti.
  Tatizo lako linaweza kuwa linatibiwa na mojawapo tu ya compounds iliyomo (dawa) kwenye mzizi, lakini sasa kwa kuwa haijawa extracted inabidi unywe na zile compoun zingine ambazo kwa kweli huzihitaji na nyingine ni SUMU.
  Matokeo yake ni kwamba unaweza kuathiri ini lako.
  Dawa za hospitali huwa zimeshafanyiwa utafiti wa kutosha na ni ile dwa unayohitaji tu ndio unapewa.
  Sipingi mizizi lakini ujue pia kun risk ya aina fulani.
  Nakutakia matibabu mema.
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  @fadhili paulo Mkuu asante kwa kunisaidia nilikuwa sipo ninaswali sasa nimesha maliza maombi yangu. Ni kuwa inategemea ni mzizi gani unaotaka kutumia wewe na je kwa maradhi gani

  yaliyokusibu wewe mpaka ukapewa ushauri wa kwenda kutumia dawa za mizizi za Wamasai? kama alivyo kuuliza swali Mkuu Fadhili Paulo na mimi nimekuuliza hivyo hivyo swali langu naomba unijibu. Zipo baadhi dawa za mizizi yenye sumu haifai kuwa ni dawa. Kwa Ushauri

  wangu unapokuw ana Maradhi kwanza nenda hospitali kafanye uchunguzi kw akina kisha tumia dawa za Hospitali ukiona hujapona njoo hapa ueleze matatizo yako utajibiwa na kupewa ushauri na kupona akipenda Mwenyeezi Mungu.

  @Fofader Mkuu jaribu uwe mkweli unachozungumza Dawa nyingi za Hospitali zina madhara kwa mwili wa binadamu kuliko Dawa za mizizi za kienyeji. Fanya utafiti kisha uzungumze sio kuponda dawa zetu za asili mkuu jaribu kuwa ni mkweli.
   
 6. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri, vipi kuhusu mizizi kuwa na uwezo wa kuimarisha misuli ya mwili kwa ujumla?? Huo uwezekano upo??
   
 7. U

  Uncle Jei Jei JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,203
  Likes Received: 944
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru kwa maelezo yako mazuri, vipi kuhusu mizizi kuwa na uwezo wa kuimarisha misuli ya mwili kwa ujumla?? Huo uwezekano upo??
   
Loading...