Utu upo wapi? Taifa tunaangamia

chidy abidal

Member
Mar 4, 2015
6
4
Je, huku ndipo tulipofika?? Je kuna matumaini yeyote tuyaonayo mbele??

Nianze kwa kumshukuru Mungu mwingi wa Rehema na mwenye kurehemu kwa kuendelea kutupa pumzi hii ya bure pasipokulipia gharama yeyote. Ama hakika ni jambo la furaha sana kwetu tuliojaaliwa kuiona hii siku mpya.

Furaha hii niliyonayo imekatishwa baada ya kusikia kuna mashabiki wenzangu wa klabu ya Yanga na pia ni Watanzania wenzangu wamepata ajali wakati wakiwa safarini kuelekea Jijini Mwanza kushuhudia mtanange dhidi ya Pyramids FC ya Misri unaopigwa pale CCM Kirumba katika Jumapili tulivu ya Tarehe 27/10/2019.

Katika pitapita zangu katika mitandao ya kijamii kama kawaida yangu ili niweze kujifunza mapya lakini pia kujamiiana na Watanzania wenzangu na duniani nikaamua kuingia mtandao pendwa wa Twitter.

Hamadi!! Ile kufungua tu nakutana na post ya kijana mmoja akiwa kapost picha za ajali na akifurahia wale watu kupata ajali na anaomba wakafie hospital maana ni kiherehere chao kwenda kuangalia mechi hiyo!! Ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni. Nikasema ngoja niendelee!! Nikaamua kuzama sehemu ya maoni (comments section) kusoma nini watu wamechangia.

Kutoka kwa mmoja wa watoa maoni ilikuwa akimkumbusha aliyeweka tweet hiyo mtandaoni kuwa yeye ni mwalimu wa sekondari na huenda wapo wanafunzi wake wenye simu janja na wanaona kile alichochapisha mitandaoni na hakitokuwa funzo jema kwa wale vijana!!

Nilistaajabu zaid mno baada ya kugundua hilo!! Maana navyotambua kwamba walimu siku zote huwa ndio viongozi wa maadili, udugu na kuinyoosha jamii hasa pale inapotetereka ukizingatia nchi yetu ya Tanzania kupitia mwalimu ndio alichagiza kupata uhuru wa iliyokuwa Tanganyika!! Lakini nikasema ngoja nisome alichomjibu huenda alitambua kakosea!! La haula !! Nikakutana na sentensi "Unafiki kwangu mwiko, mimi ni Simba na siipendi Yanga, kama ni kufa wafe tu naona wanachelewa sana"

Nilistuka mno maana nilitegemea maoni ya aina hii yangepatikana kwenye mijadala ya kisiasa kama ilivyotokea wiki iliyopita!! Chuki imekuwa ni kubwa sana.

Watu wanasahau mpira ni burudani. Mpira ni starehe lakini mwalimu tena wa sekondari kufikia kuonesha mawazo yale niliogopa mno Ni kizazi gani atatuletea endapo akapata japo ukuu wa shule, uafisa elimu wa wilaya au mkoa ama uongozi wa nchi!!

Ni wapi tumekosea!! Je, ni kwamba elimu yetu imelega mno mpaka walimu kufikia hatua hiyo!! Kwa nini umoja wa kitaifa unalega!! Je, utu ndio ulikwenda na upepo wa kisulisuli uliovuma wiki zilizopita!!

Usinijibu mimi!! Baki na majibu yako!! Chukua hatua kwa jamii uliopo.

Natua kalamu yangu

1996rashidi@gmail.com
 
Back
Top Bottom