UTU na UMUHIMU WA KURIPOTI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTU na UMUHIMU WA KURIPOTI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaNanii, Aug 24, 2012.

 1. K

  KakaNanii JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Sep 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  [FONT=&amp]
  Wiki hii Mkuu wa Mkoa wetu wa Pwani Hajjat Mwantumu Mahiza alizungumza na waandishi wa habari na kuelezea masikitiko yake kwa binaadamu ambao wamekuwa wakitanguliza sifa na maslahi binafsi badla ya utu pale wanaposhughulikia majanga mbalimbali ikiwemo ajali.

  Hajjat Mahiza ametoa kilio chake kutoka na kuwa mkoa wetu wa Pwani umekuwa ni muhanga wa matukio mbalimbali[/FONT]
  [FONT=&amp]ya ajali ambapo wanaofika eneo la ajali badala ya kushirikiana kuwasaidia wahanga au manusura wa ajali basi watu hufanya vitendo vya uhalifu kama kuwahi kuiba MALI au 'ngawira', na wengine kujihusisha na kuchukua PICHA za tukio zinazoonesha hali ya mambo ili waziuze kwenye vyombo vya habari.

  Tabia hii imeota mizizi siku hizi ambako maendeleo yamekuwa makubwa katika kupashana taarifa. Bi Mwantum Mahiza ametoa wito kwa watanzania kuacha tabia hizo na badala yake wajenge tabia ya kutanguliza UTU kuwasaidia wanaokutwa na matatizo.[/FONT]
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  assalaam alaikum hajjat, ahsante kwa kutukumbusha.
   
Loading...