chupaki chupaki
Member
- Jul 4, 2017
- 7
- 0
Mh.Rais kwa heshima kubwa nakupa pongezi kwa namna unavyoliongoza taifa letu.Mimi ni mkopaji tangu mwaka 2014 katika kampuni hii changa ya umma iliyoaanzishwa mwaka 2013 nasikia ipo chini yawizara ya fedha.
Ninawakilisha wana kikundi 256 tuliopo hapa Ngarenaro Arusha na wenzetu wapo 104 Mbagala Dar es salaam.
Tulikopa kupitia kampuni hii ya umma na tuliweka dhamana zetu mamilioni ya shilingi kwa pamoja lakini mpaka sasa imekuwa ni kilio kikubwa.
Licha ya kuwa kampuni haikopeshi tena mikopo mipya tangu mwaka jana kutokana na tatizo kubwa la ukwasi lakini pia Hatujarejeshewa pesa zetu za dhamana ambazo tulikuwa tunaweka.
Kwa kila mwanakikundi alitakiwa kuweka mpaka asilimia 25 kama dhamana lakini mpaka leo kampuni inakaribia kufa hatujalipwa pesa zetu.
Tunaambiwa na wenzetu walioko dar slam kilio chao pia hakisikilizwi kutokana na kwamba kampuni haina pesa,iko taabani kiuchumi na mikopo ya vikundi haitolewi mpaka karibuni hapa waliposaidiwa pesa na kampuni fulani ya GEPF.
Kuna taarifa kuwa kampuni pia haikopesheki haikopesheki kwenye mabenki hiyo inatokana na wao viongozi kutafuna hela zetu.Pia wameshindwa kulipia pango kwenye ofisi zake nyingi na wamefukuzwa hivyo hali hii inatutisha.
Tungependekeza uwabane viongozi wao ili waturudishie hela zetu.Japo ile ya vipande UTT AMIS tunasikia bado iko vizuri sana...Mungu aubariki uongozi wa hao wa vipande waendelee hivyo hivyo.
Hans Kibola yule mkurugenzi wa UTT AMIS yuko vzuri na Mungu akulinde uendelee kuilinda UTT AMIS.
Tunakuomba Mh Rais utusaidie sisi wanyonge