CAG Ludovick Utouh: Kigogo Epa alitenga rushwa bil.30/-

CAG Ludovick Utouh: Kigogo Epa alitenga rushwa bil.30/-

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyestaafu Ijumaa iliyopita, Ludovick Utouh, amefichua kuwa mmoja wa watu waliohusika katika kashfa ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) alitenga rushwa ya Sh. bilioni 30 kwa nia ya kuipata ripoti ya ofisi yake kwenda serikalini.

Akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE yaliyofanyika kwenye ofisi yake jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya kustaafu rasmi, Utouh alisema kuwa kwa bahati alipata taarifa za kuwapo kwa mpango wa kuwapo kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotengwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha jaribio la kuifikisha ripoti ya CAG kwa kigogo huyo wa EPA kabla ya kwenda serikalini na kumfikia Rais Kikwete, hivyo yeye akajikuta akiwa na hofu kubwa.

"Nilipata ripoti wakati wa EPA kwamba kuna mtu aliyekuwa ame-set aside (ametenga) bilioni 30 kwa mtu yeyote ambaye angempatia ripoti yangu mimi kabla haijaenda serikalini. Nilipata hiyo ripoti... sasa unapopata ripoti kama hiyo... unakuwa na wasiwasi," alisema Utouh.

Akieleza zaidi, Utouh alisema kuwa kutokana na uwapo wa tishio hilo, alilazimika kuchukua tahadhari ya ziada na kwamba kuna wakati alikuwa akijifungia ofisini muda wote kwa nia ya kujiweka salama na kwamba hata alipokuwa barabarani, muda wote alikuwa katika tahadhari kubwa.

"Mimi nilikuwa najifungia hapa ofisini kabisa kwa sababu, unajua na-make sure (nahakikisha) milango yote imefungwa. Ukitembea, ukiona gari inakuja, unamwambia dereva aangalie. Ilikuwa tension kali sana. Yaah... ni tension kali sana," alisema Utouh.

CAG huyo mstaafu alifichua ukweli huo baada ya kuulizwa ni wakati gani hasa ambao aliwahi kuishi kwenye mazingira magumu ya kiutendaji katika miaka yake minane ya kuwa na madaraka ya CAG.

"Ukweli ni wakati wa ukaguzi wa EPA... ilikuwa inasemwa sana kwenye vyombo vya habari. Ikaandikwa sana. Halafu kukawa na hisia.

Watu wanazungumza, hii ni ya fulani, sijui ya fulani, sijui ilifanyaje... sasa kwa hiyo unapokuwa katika hali ya aina hiyo... mhh - mhh - heh! Hujui sasa anayekuandama. Hujui anayekutafuta," alisema Utouh.

Sakat la EPA lilihusisha wizi wa takriban Sh. bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania.

Watu kadhaa wameshafikishwa mahakamani kutokana na kashfa hiyo, wengine wakifungwa na kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 60 kikirejeshwa na watu waliokwapua fedha hizo na kutumiwa na serikali kusaidia sekta ya kilimo kupitia dirisha maalum lililofunguliwa kwenye benki ya TIB.

CHANZO: NIPASHE
 
Huyo kigogo alitakiwa ajulikane na akamatwe wakati huo kama Utoh angetoa taarifa. Sijui ni kwanini wastaafu wengi huficha habari muhimu na kuja kuzitoa baada ya kustaafu wakati huo taifa limeumia.

Hata yule mkurugenzi wa misitu naye alisema hivyo hivyo kuwa alitengewa mamilioni akakataa. kwanini huwa hachukui hatua wakiwa madarakani? Sasa Utoh atwambie wale ambao rais alidai atawasamehe wakirudisha na akina nani walirudisha na wale ambao hawakurudisha na hatu ambazo rais alichukuwa.

Tafsiri rahisi hapa ni kuwa anayesamehe ni mshirika wa wizi huo. Kwanini awasamehe na ni kwa sheria ipi na ni kwanini aliaowasamehe iwe siri yake.

Mbona akisamehe wafungwa huwa wanajulikana na kutangazwa kwanini iwe wa EPA? Ni lazima mtu awe amenufaika kwa namna moja au nyingine ndipo anaweza kuchukua maamuzi hayo.
 
lol, kumbe nido maana hawa jamaa walisamehewa na kuombwa warudishe cheque (sio fedha kama alivyowahi kutaka Mama Kilango kuziona zikiwa kwenye viroba)!
 
Hii nchi kweli imeoza? Hawa viongozi ni kuchota hela na kigawa rushwa sana
 
Huyu utouh mwongo mkubwa,yaani mtu atenge bilioni thelasini kwa kesi ya bilioni mia thelasini? Anatafuta kick kwenye media, hata ripoti zake zinafanana na uongo wake ndio maana wazushi kama kina kafulila walitaka atoe ripoti zote yeye kabla ya kustaafu
 
Hii nchi inaendeshwa kimaandazi sana. Hakuna anayeheshimu utawala wa sheria.
 
kazi ya utoh sijaionea manuaa yoyote mpaka leo!
wht's your proffessioon?...so far hakuna CAG aliyefanya mazuri kama Utouh,mpeni haki yake jamani,serikali ilikuwa haiyafanyi kazi maoni yake,kwani ndio kazi yake,to give his opinion and nothing else!
 
Asema alilazimika kujifungia ofisini
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyestaafu Ijumaa iliyopita, Ludovick Utouh, amefichua kuwa mmoja wa watu waliohusika katika kashfa ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) alitenga rushwa ya Sh. bilioni 30 kwa nia ya kuipata ripoti ya ofisi yake kwenda serikalini.

Akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE yaliyofanyika
kwenye ofisi yake jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya kustaafu rasmi, Utouh alisema kuwa kwa bahati alipata taarifa za kuwapo kwa mpango wa kuwapo kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotengwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha jaribio la kuifikisha ripoti ya CAG kwa kigogo huyo wa EPA kabla ya kwenda serikalini na kumfikia Rais Kikwete, hivyo yeye akajikuta akiwa na hofu kubwa.

"Nilipata ripoti wakati wa EPA kwamba kuna mtu aliyekuwa ame-set aside (ametenga) bilioni 30 kwa mtu yeyote ambaye angempatia ripoti yangu mimi kabla haijaenda
serikalini. Nilipata hiyo ripoti... sasa unapopata ripoti kama hiyo... unakuwa na wasiwasi," alisema
Utouh.

Akieleza zaidi, Utouh alisema kuwa
kutokana na uwapo wa tishio hilo,
alilazimika kuchukua tahadhari ya ziada na kwamba kuna wakati
alikuwa akijifungia ofisini muda wote kwa nia ya kujiweka salama na kwamba hata alipokuwa barabarani, muda wote alikuwa katika tahadhari kubwa.

"Mimi nilikuwa najifungia hapa ofisini kabisa kwa sababu, unajua na-make sure (nahakikisha) milango yote imefungwa. Ukitembea, ukiona gari inakuja, unamwambia dereva aangalie. Ilikuwa tension kali sana.

Yaah... ni tension kali sana," alisema
Utouh.

CAG huyo mstaafu alifichua ukweli huo baada ya kuulizwa ni wakati gani hasa ambao aliwahi kuishi kwenye mazingira magumu ya kiutendaji katika miaka yake minane ya kuwa na madaraka ya CAG.

"Ukweli ni wakati wa ukaguzi wa EPA... ilikuwa inasemwa sana kwenye vyombo vya habari. Ikaandikwa sana. Halafu kukawa na hisia.

Watu wanazungumza, hii ni ya fulani, sijui ya fulani, sijui ilifanyaje... sasa kwa hiyo unapokuwa katika hali ya aina hiyo... mhh - mhh - heh! Hujui sasa anayekuandama. Hujui
anayekutafuta," alisema Utouh.

Sakata la EPA lilihusisha wizi wa
takriban Sh. bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania.

Watu kadhaa wameshafikishwa
mahakamani kutokana na kashfa hiyo, wengine wakifungwa na kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 60 kikirejeshwa na watu waliokwapua fedha hizo na kutumiwa na serikali kusaidia sekta ya kilimo kupitia dirisha maalum lililofunguliwa kwenye benki ya TIB.

CHANZO: NIPASHE
 
Good riddance Ludovic Utuoh; ulikuwa CAG mzigo; tangu ulipowatetea Richmond na kumsafisha David Jairo nilipoteza imani na wewe; A good for nothing CAG
kazi ya utoh sijaionea manuaa yoyote mpaka leo!
 
hivi zilizorudi jumla mpaka sasa ni shingapi?
sidhani kama hili swali lijibiwa
 
Ilimbidi awe na tahadhari kubwa kwa sababu aliemtuma kukagua na ndio huyohuyo atakaempa ripoti ya ukaguzi huo na ndio huyohuyo mtuhumiwa namba moja wa ufisadi huo. Hii maana yake mtuhumiwa anakupa kazi ukamchunguze..........
 
kitendo cha cag kuto toa taarifa police ili wafanye uchunguzi ni dhahiri alisaidia uhalifu, nchi za wenzetu angeshtakiwa!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mzee kafanya kazi kubwa akatulie ale pension yake ya uzeeni.
 
Hah! Tanzania zaidi ya uijuavyo. Anaongea haya baada ya kustaafu madaraka. Anaweza kutuambia alizopewa akakubali pia? Sidhani.
 
Back
Top Bottom