Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,079
- 9,245
Porojo za Kijinga hizi , na unaweza kumdanganya darasa la chekechea tu, au wajumbe wa sasa wabunge la katiba walioko kule doodma, maana wao ndio hawatumii kichwa kufikiri.
Zitarudi vipi wakati mwenye kusamehe ndiye mnufaika mkuu? Itatakuwa ajabu mwizi aliyeiba chakula kwa mkono wa kulia halafu aukate mkono huo kwa kutumia mkono wa kushoto baada ya kushiba! Is it possible???!!!hivi zilizorudi jumla mpaka sasa ni shingapi?
sidhani kama hili swali lijibiwa
Ajabu! Mwizi anaiba halafu anatuma watu wafanye uchunguzi kisha ripoti ya wizi inapelekwa kwa mwizi mwenyewe!Huko alikopeleka hiyo Report ndiko hukohuko fedha hizo zitapokelewa na hatutaona kamwe hatua zozote kuchuliwa.
Yaani wazee kama hawa kama anaongea mbele ya mtu mwenye welewa unaweza kukuta unammamata vibao kwa hasira. Haya mazee yakistaafu ndio utasikia "nilikataa milioni 30" mwingine "nilitaka kuhongwa gari nikakataa" mwingine "nilikataa bilioni 30" na ujinga mwingine mwingi yakifikiri kwa kusema hivyo ndiyo yatasifiwa kwa kukataa rushwa. Kwa kiongozi thabiti huyo anayetaka kutoa bilioni 30 tayari ni ushahidi tosha kuwa ndiye mwizi hivyo anawekewa mtego anakamatwa na kuozea ndani na bilioni 30 inachukuliwa kwa shughuli za maendeleo. Sasa si ajabu hata huyo aliyetaka kutoa bililoni 30 yupo mtaani anatanua na bilioni zake 30 maana hazikuchukuliwa. Yaani wazee kama hawa hata wangepelekwa Mabwe pande halali yao. Unaeleza ujinga ukitegemea sifa?! Wakati mwingine bora wangekuwa wananyamaza ili tuwasahau polepole lakini sasa ndio wanajivua nguo kuwa kumbe walikuwa wa hovyo kabisa!Kwanini hakusema wakati huo? Sasa anasema wakati ameshastaafu huku akificha jina la huyo muhusika ili iweje? Huyu naye ni fisadi tu!!!
Excellent! Hakuna cha kuongeza wala kupunguza hapo!Ilimbidi awe na tahadhari kubwa kwa sababu aliemtuma kukagua na ndio huyohuyo atakaempa ripoti ya ukaguzi huo na ndio huyohuyo mtuhumiwa namba moja wa ufisadi huo. Hii maana yake mtuhumiwa anakupa kazi ukamchunguze..........
Mwizi kajileta mwenyewe na bil. 30 halafu unanyamaza na kujifungia ndani. Ndio akili hiyo? Hiyo ndiyo profession yake kwamba katika uchunguzi wa kihasibu anapojitokeza mwizi wa ulichokuwa unachunguza unafichama na yeye kumfichia siri? Kwenye hiyo opinion yake aliiambia serikali kuwa kuna mtuhumiwa alitaka kuhonga bil 30 illi hatua zichukuliwe? Wewe ulishasikia serikali imemkamata mtuhumiwa wa EPA aliyetaka kuhonga bil 30 ili kupoteza ushahidi? Sasa alikuwa anachunguza nini kama alishindwa kufichuwa mpango wa mtuhumiwa huyo anakuja kusema leo wakati kastaafu na hatwambii huyo mtu ni nani na kwanini na yeye anamficha kama yule aliyeamua kuwasamehe wezi wengine wa EPA na kufanya siri yake. Obviously huyo naye atakuwa mwizi mwenzao. Huyu mzee sijui nani kamshauri aje hadharani na ujinga huu?wht's your proffessioon?...so far hakuna CAG aliyefanya mazuri kama Utouh,mpeni haki yake jamani,serikali ilikuwa haiyafanyi kazi maoni yake,kwani ndio kazi yake,to give his opinion and nothing else!
Unapenda kutaja taja majina wakati hata ukitajiwa huwezi kufanyia kazi.
Huyo kigogo alitakiwa ajulikane na akamatwe wakati huo kama Utoh angetoa taarifa. Sijui ni kwanini wastaafu wengi huficha habari muhimu na kuja kuzitoa baada ya kustaafu wakati huo taifa limeumia.
Hata yule mkurugenzi wa misitu naye alisema hivyo hivyo kuwa alitengewa mamilioni akakataa. kwanini huwa hachukui hatua wakiwa madarakani? Sasa Utoh atwambie wale ambao rais alidai atawasamehe wakirudisha na akina nani walirudisha na wale ambao hawakurudisha na hatu ambazo rais alichukuwa.
Tafsiri rahisi hapa ni kuwa anayesamehe ni mshirika wa wizi huo. Kwanini awasamehe na ni kwa sheria ipi na ni kwanini aliaowasamehe iwe siri yake.
Mbona akisamehe wafungwa huwa wanajulikana na kutangazwa kwanini iwe wa EPA? Ni lazima mtu awe amenufaika kwa namna moja au nyingine ndipo anaweza kuchukua maamuzi hayo.
mbona wengi tu tupo ccm na ni masikini wa kutupwa au tunaishi kwa kazi za wazi!!! tuanze kutenganisha wezi na ccm huko kujumlisha ndo kunaifanya ccm iwe na nguvu kwa sababu mnawaamsha wale waadilifu waliomo ndani..we taja jina la mtu aliyetajirika kupitia ccm ndo tu-deal naye..Ukiwa CCM usipokuwa tajiri basi wewe ni mpuuzi wa kutupwa. Nimejisemea tu
Hiyo ni fiction. Unauhakika gani kuwa zilirudi? Na kwanini hazikupangiwa matumizi na bunge? Ni akina nani hao waliorudisha? Je walirudishaje na kwa nani? Ni akina nani hawakurudisha na hatua gani zimechukuliwa dhidi yao? Na ni kwanini rais awafanye siri wakati pesa zilizoibwa ni za umma na si zake binafsi? Hiyo utaratibu wa msamaha kwa wezi ni kwa sheria zipi za nchi? Hiyo busara lazima iwe na manufaa kwake vinginevyo hakuna ukweli wowote. Angefanya hivyo kwa mali yake binafsi aliyoibiwa hatuna shida! Huyo bwana yumo kwenye list of shame na hajawahi kukanusha wala kujitetea. Hivyo hao aliodai "kuwasamehe" ni wenzake!Hela zimeibiwa Rais ametumia Busara zimerudishwa zaidi ya 60b . Nadhani Rais anastahili pongezi vinginevyo hadi leo tungekua tunalumbana nao mahakamani , wakipatikana na hatia Hakimu angehukumu 'jela miaka 7 ukitoka ulipe hela ulizoiba'!
Huyo kigogo alitakiwa ajulikane na akamatwe wakati huo kama Utoh angetoa taarifa. Sijui ni kwanini wastaafu wengi huficha habari muhimu na kuja kuzitoa baada ya kustaafu wakati huo taifa limeumia.
Hata yule mkurugenzi wa misitu naye alisema hivyo hivyo kuwa alitengewa mamilioni akakataa. kwanini huwa hachukui hatua wakiwa madarakani? Sasa Utoh atwambie wale ambao rais alidai atawasamehe wakirudisha na akina nani walirudisha na wale ambao hawakurudisha na hatu ambazo rais alichukuwa.
Tafsiri rahisi hapa ni kuwa anayesamehe ni mshirika wa wizi huo. Kwanini awasamehe na ni kwa sheria ipi na ni kwanini aliaowasamehe iwe siri yake.
Mbona akisamehe wafungwa huwa wanajulikana na kutangazwa kwanini iwe wa EPA? Ni lazima mtu awe amenufaika kwa namna moja au nyingine ndipo anaweza kuchukua maamuzi hayo.
Mwizi kajileta mwenyewe na bil. 30 halafu unanyamaza na kujifungia ndani. Ndio akili hiyo? Hiyo ndiyo profession yake kwamba katika uchunguzi wa kihasibu anapojitokeza mwizi wa ulichokuwa unachunguza unafichama na yeye kumfichia siri? Kwenye hiyo opinion yake aliiambia serikali kuwa kuna mtuhumiwa alitaka kuhonga bil 30 illi hatua zichukuliwe? Wewe ulishasikia serikali imemkamata mtuhumiwa wa EPA aliyetaka kuhonga bil 30 ili kupoteza ushahidi? Sasa alikuwa anachunguza nini kama alishindwa kufichuwa mpango wa mtuhumiwa huyo anakuja kusema leo wakati kastaafu na hatwambii huyo mtu ni nani na kwanini na yeye anamficha kama yule aliyeamua kuwasamehe wezi wengine wa EPA na kufanya siri yake. Obviously huyo naye atakuwa mwizi mwenzao. Huyu mzee sijui nani kamshauri aje hadharani na ujinga huu?