Utoro wa walimu unatugharimu zaidi ya mara mbili ya pesa za Escrow kwa mwaka

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
Kila mwalimu wa darasa la 1 hadi 3 hugharimu shilingi milioni tisa (kabla ya kodi)

Kuna walimu 191,604 (wa darasa la 1 hadi 3) kwenye shule za msingi za serikali nchini. Kila mwaka walimu hao hulipwa shilingi bilioni 1,724.

Screenshot from 2017-05-29 16-28-04.png


Kutokana na takwimu za KiuFunza kwa wastani, 46% ya walimu hawapo darasani ama shuleni hivyo Shilingi bilioni 793 hupotea kila mwaka, shilingi milioni 4.1 kwa mwalimu

Pesa hizi zina thamani zaidi ya mara mbili ya pesa za Escrow.

Chanzo: Utafiti wa KiuFunza 2016
 
Mi nilizoea kuwa wanafunzi ndo wanakuwa WATORO,kumbe hadi waalimu???Haya ni maangamizi ya taifa.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tafiti za uchonganishi.. Kuna Mwalim anaeweza kuwa kituoni asiingie darasani.. Labda aingie darasani asimalize mada za masomo
Nadhani watu wote tumesoma atleast shule ya msingi humu ndani na tunajua kabisa kuwa kuna walimu huwa hawafuati ratiba. Unakuta muda wa kipindi anajaza sijui fomu gani au attendance za wanafunzi.
 
Nahisi kama wangewekewa mazingira mazuri ya kufanyia kazi...utoro usinge kuwepo sio shule za msingi tuu hata shule za secondary...tatizo ni mazingira ya kufanyia kazi na mishahara kama mwalim asipo jiongeza yeye mwenyewe nahisi hata nguo za kubadili atakosa. Swala kubwa hapa ni kuangalia je ni mazingira gani hawa walimu wanafanyia kazi na je huo mshahara wanao pewa unakizi mahitaji yao.
 
Ni kweli utoro wa kutokamilisha ufundishaji upo ila shuleni kuna majukumu lukuki ambayo ni muhimu na mwl asipoyaacha kwa muda ili afundishe inaweza kuwa ni tatizo: Mfano, unakuta mwl ana vipindi Vinci wakati huohuo anashughulikis fedha za SHULE kama mhasibu kwa hiyo vipindi vyake vingi hupotea wakati anashughulikis masuala ya fedha.
Hawa jamaa WA utafiti ningewaona WA maana sana kama wangetafiti namna ya kummotisha mwl ili atimize majukumu take vyema kwa sababu kuwa darasani tu hakuna maana ya kufundisha,unaweza kumkuta mwl kwenye mazingira ila darasani shughuli zinaendelea.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
KiuFunza? Nawaza tu, kwanini "F" imeandikwa kwa herufi kubwa ktk hao watafiti.
 
Ni sahihi tuu kazi kubwa mshahara kiduchu na mitusi juuuuuuu, wacha na wao wakasake tonge maana sirikali kama vile hawasikii vilio vyao,kazi lukuki malipo haba
 
Wanaposikia mara memeta mara Richmond, mara mchanga wa dhahabu.
Waalimu wanavunjika Moyo,
Wanaona bora wawe watoro waka uze maandalizi .
Kwa hali Kama utaongoza Kwa shida sana
 
Tatizo letu liko hapo, tuongezewe mshahara kwa matunda yapi?
Kufanya wajibu wako mpaka upewe motisha. Swali rahisi tu, hiyo motisha itoke wapi wakati wewe huzalishi mali au unarudisha nyuma utoaji huduma?
Kama malipo hayatoshi kabisa tuache kazi au tudai chetu(sijasema tuombe).
 
Back
Top Bottom