Utofauti wa Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye katika mambo mbalimbali

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Kwanza mjue cheo ni dhamana kubwa hata unapotolewa unaumia,

Mwigulu ni mtu aliyekulia mazingira magumu sana na anajua matatizo muhimu ya watanzania kwa kuyaishi, wakati Nape kakulia kwenye familia inayojiweza kiuchumi, na ameyajua matatizo ya watanzania kwa kuyaona tu,

Mwigulu ni genius sana hata ukifuatilia history yake uko nyuma, tofauti n.a. Nape yeye amebobea katika siasa hajawahi kuyafanya maajabu yeyote kitaaluma,

Mwigulu alijua mapema kwamba uwaziri si lazima ndo maana baadhi ya mambo alikaa kimya refers barua ya maaskofu na waraka, au pale aliposhinikizwa na Wana CCM kuchukua hatua kali juu ya wapinzani, ila nape aliumia sana na alijiona anaweza kukosoana na mkuu wake wa kazi juu ya sakata la Makonda,

Mwigulu hana kinyongo na mtu na ukisikia hotuba zake zinakuwa zimejikita zaid katika masuala ya kawaida ila nape hotuba zake Nyingi utasikia mbegu niliyopanda imeoza na inataka kuota huku akilia,

Mwigilu hana mzizi mrefu ndani ya Chama lakin Nape anasapoti kubwa ya kina mwandosya, kikwete na Waandamizi wakubwa,

Mwigulu Nchemba ni mtu aliyezungukwa na aliyajiweka karibu na washauri wazuri, na anajua kuusoma upepo, ila nape upepo wake hajui kuusoma ye anaenda kifua mbele bila kujua impact zake,

Mwigulu hajalelewa n.a. deko,ila nape maneno yake na ushikaji wa maiki inaashiria kuwa ana deko fulani

Nape anaijua sana CCM kuliko Mwigulu

Mwigulu hampi sana headache Magufuli kama alivyo nape, anampa Magufuli headache sana,

Mwigulu ana nafasi ya kuja kuwa kiongozi mkubwa baadae ila Nape inabidi struggle sana,

Ongeza nyingine,
 
Mwigulu ni zaidi ya kiongozi, ni moja ya vijana Bora sana kuwahi kutokea,ninasema kutoka moyoni siku moja Dr Mwigulu Nchemba ataiinua Tanzania,namuona juu kabisa kabisa anajua kutumia vizuri maarifa,ni mtu wa watu,hata iwe jua na giza siku moja atasimama kama kiongozi mkuu wa nchi hii,tunampenda sana sisi vijana mpaka wazee
 
Makamba naye anaandaliwa kuchinjwa ili mkuu wa region hasiwe na mpinzani ndani ya upepo wa feri cc@Pascal Mayalla
Kamwe halitatokea.
Ile wizara kaimudu, kelele za muungano, na mazingira zimepungua.

Alafu yuko chini ya Makamu Rais, so lazima ashauriane na Mama kwanza na ampe sababu.

Pia Makamba anajua kucheza na aina ya mtu. Huwezi sikia kafanya lolote baya kumchukiza Magufuli.

Nafikiri ndie Rais Ajae.
 
Kamwe halitatokea.
Ile wizara kaimudu, kelele za muungano, na mazingira zimepungua.

Alafu yuko chini ya Makamu Rais, so lazima ashauriane na Mama kwanza na ampe sababu.

Pia Makamba anajua kucheza na aina ya mtu. Huwezi sikia kafanya lolote baya kumchukiza Magufuli.

Nafikiri ndie Rais Ajae.
Hana uwezo wa kuwa rais
 
Back
Top Bottom