Utoaji bastola Wa aina ile ni Wa hatari ukemewe.

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
300
423
Nimeangalia video inayozunguka mitandaoni ikimuonyesha MTU ambaye haijatambulika kuwa ni nani akimtolea bastola aliyekuwa waziri wa mambo ya habari na utamaduni Mh. Nape .

Nimefurahi kwamba kama wale ni watu Wa usalama walikua kazini kuhakikisha Usalama Wa Nchi yetu .

Ni lazima tuwapongeze na tutembee kifua mbele kwamba ulinzi wetu uko makini kuhakikisha mambo yanaenda inavyopaswa.

Lakini nimepatwa na maswali ya kujiuliza kwa aina ile ya utoaji Wa silaha ile kwa MTU asiyekua na silaha je ni sahihi?

Na kama huyo MTU angekua ameshikilia silaha katika mfuko Wa suruali yake he kwa kujizungusha kule kutoa silaha upande Wa kushoto tena na mkono Wa kushoto ndio uipeleke mkono Wa Julia si utawahiwa?

Kuna haja ya kuendelea kuwanoa zaidi kama ndio watu Wa aina ile ndio tunawategemea huku tukiendelea kuuza aina hiyo ya silaha huku mtaani.

Wasijisahau wakifikiri hizo silaha ni wao pekee ndio wanamiliki hiyo itawagharimu pakubwa.

Katika hali ya kawaida MTU hutakiwi kutoa silaha na kulenga MTU au kitu chochote kama hujadhamiria kudhuru huyu yeye hajui kwamba silaha ile ni hatari?

Weledi uzingatiwe katika kazi tufanyazo.
1490401745413.jpg
 
Huhitaji kuwa mtaalam wa silah kujua ule utoaji wa silaha, kuihamisha mkono mwingine na alivyoishika una walakini mkubwa!
 
Huyu anapenda kushoto zaidi.. si unaona mfuko wake wa nyuma kushoto pia kaweka pingu?
 
Back
Top Bottom