Utitiri wa shule za "English Medium" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utitiri wa shule za "English Medium"

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ngoshwe, May 14, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  May 14, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Nukuu hii hapa chini ni malengo makuu ya kuanzishwa kwa shule ya Southern Highlands School inayotoa elimu kwa kufuata mtaala wa lugha ya Kiingereza (English Medium School).Shule hii inamilikiwa na familia ya Mhe. Mungai ambae alipata kuwa Waziri wa Elimu wa nchi hii.
  Ki mtazamo, inaonekana kana kwamba shule nyingi za "English Medium" zimekuwa zikianzishwa kwa madhumuni makubwa ya kuwajenga vijana wetu kufahamu kiingereza zaidi lakini wakati huo huo tunahimiza matumuzi ya kiswahili chetu.

  Uzoefu pia unaonyesha kuwa kwa sasa shule nyingi zimekuwa zikitumia hilo neno "English Medium" kuvuta wazazi wengi kupeleka watoto wao huo.. Laikini binafisi sina uthibitisho wa kutosha kuhusu viwango vya taaluma inayotolewa kupitia lugha hiyo ya Kiingereza ambacho kwa shule nyingi imekuwa ikifundishwa na wageni kutoka Kenya au Uganda na si Watazania japo kuwa wpo wale ambao wamemaliza katika shule hizi hizi za Kiingereza!.

  Kwa wale wenye uzoefu na shule hizo labda watusaidie kiwango cha taaluma kinachotolewa na shule hizo mbali na suala la watoto kujua lugha ya Kiingereza!!.


   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  May 14, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwani tatizo liko wapi, nawee ukitaka si ujenga yako? kama huna pesa za kujengea waache wenye nazo wajenge ili watoto wa kitz wafaidi. wivu tuuu wivu tuuu kila mkiona mtu anafanya kitu cha maana.
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  May 14, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Kiwango cha taaluma kinategemea ni shule ipi unayoiongelea, hauwezi ukatoa comment kuhusu shule zote za English medium kwa pamoja.
   
 4. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kuwa utitiri wa shule za English medium ni ushamba wa waswahili tu.Hata sisi tunaoanzisha wengine wala hatukithamini kiiengereza lakini tunafanya hivyo kuwavutia wazazi wa watoto wanaofikiri mtoto wao akizungumza kiiengereza kama mkoloni ndio mwisho wa matatizo.
  Mimi nina shakaa na watendaji wa wizara ya elimu tangu zamani kwamba huwa wanahongwa na waiengereza na wafaransa ili lugha zao zifundishwe mashuleni.
  Fitina ya umuhimu wa kiteknolojia juzi imezimwa baada ya mitandao ya intaneti kuanza kutumia hata herufi za lugha nyengine kama kiarabu bila hata herufi moja ya kiiengereza.Sasa watoto walioko arabuni au China wana ulazima gani kusoma kiiengereza?.
   
 5. k

  kiber Member

  #5
  May 15, 2010
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huu ni ujinga uliyokomaa TZ. kuna jirani yangu aliwapeleka watoto wake kusoma Nairobi miaka ya 90, ni tajiri sana an mihela kibao, watoto waliporudi likizo kiswahili washasahau na wazazi wao hawajui hata kuongea kithungu, ehh mbona aliwarudisha TZ kwani ilikuwa taabu sana! fuata mkumbo!
   
 6. O

  ODILI SAMALU JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2014
  Joined: Dec 13, 2013
  Messages: 1,261
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  zinasaidia watoto kujua kingereza
   
Loading...