Jisemee wewe binafsi na nafsi yako ila usiwasemee wenzako huku nje tunaokutana nao wanaitafuta ndoa kuliko hata kazi na wengine wapo makazini ila huwaambii kitu kuhusu ndoa wanataka hata ya bahati mbaya.
Ndoa anaitafuta Jennifer Lopez, anapesa na ni mzuri, sembuse ninyi ambao hata pesa ya kifurushi cha wiki kumudu ni mtihani.
Niffer yule pale ni binti mchakalikaji anakwenda Dubai, china na kwingineko ila umeona alichofanya, katafuta mwanaume amemuoa na wanapambana wote. Sasa yule ni binti anayeelewa maana na nafasi ya mwanaume hata kama anajeuri ya kutafuta pesa. We unadhani alishindwa kusema aishi kisela?
Ni akina ninyi tu ambao ni kwanza masikini wa kipato, mnatoka familia za kawaida na hamna ramani ya maisha kujifanya mnajua kupambana na huku uhalisia wa maisha yenu ni kuomba pesa tena kwa exchange ya kupelekwa location kuliwa ili mpost.
Sasa wewe kama unahisi unahiyo jeuri unayosema uko nayo nakupa hapa count down. Mwanamke una miaka 10 tu ya kuringa na kuleta mbwe mbwe za usichana, baada ya hapo utazolewa na mwanaume yoyote ambaye atakuwa available ukigoma utajiongezea mateso ya hisia na utakuja olewa na kituko cha mwanaume kuliko mwanaume uliyemdharau kuliko wote.
Hesabu miaka 10 kutokea umri wa miaka 16. kutoka 16 hadi 26 ni miaka 10 yenyewe. Sasa sijui wewe umri gani. Kama umevuka 26 then count down imeanza ukielekea 30 ambayo ni umri wa lala salama. Tafuta hela uje ulelee Marioo na wanaume za watu matapeli ila kupata mwanaume wako wa ndoto sahau utabakia kuota ila hauta muona.
Kama unabisha hata twende kazi.