Uthubutu wa Rais Magufuli...

Uthubutu wa Rais Magufuli...

I see, you're not on a straight line, but following a zigzag pattern!

What you're recommending is a sure chaos not much different from what we are about to experience as a result of the dare devil decision making from an individual.

I'll leave it at that for the moment.

Straight line has been done and again rather than awakening wananchi to do the right thing... wananchi made bad choices 2009, 2010, 2014, 2015 and so they will repeat 2019 and 2020!

Mtanzania inabidi abadilishwe mtazamo by looking inwards not outwards!

Wangapi wanajua thamani ya kura na kodi zao? Leo unapiga kura na kulipa kodi then anakuja mtu uliyemuajiri anakunyanyasa!

Uthubutu is to say NO kwenye minyanyaso... Uthubutu ni ku-demand accountability bila fear... na si kukubali kuaminishwa!

It was said it will be impossible for ATCL to have brand new planes, they have spanking new even though they don’t have meaningful business idea to run it.

Why can’t mwananchi become bold to safe guard his Kura na Kodi by demanding accountability and not caving to “nitawashughulikia?”

Leo nimeona video mkurugenzi-RAS au DAS somewhere Arusha anasema watu wapigwe pingu na anakataa kuwapa nafasi watoe maelezo. Polisi hamuulizi Mkurugenzi hii arrest ni ya sheria gani au kutokana na kosa gani kisheria ili Polisi na Jamhuri ziwe protected against false arrest and detaining... anavuta pingu... anatimiza mbweko wa amri.

We need to change, we need to ask questions bila woga, tufanye mambo bila woga wa amri na mtoa amri! Maana watoa amri wana Uthubutu wa kuvunja sheria na kanuni na wanapeta... kwa nini wapewa amri nao wasiwe na uthubutu kukataa kuburuzwa?

Yes tunahitaji Uthubutu kukataa kuburuzwa ili tunaowapa majukumu waanze kuheshimu kura na kodi zetu na kusimamia haki na kufuata sheria si kujifanyia wanalotakabkisa wana Uthubutu!
 
Mhhhh!!
Uchambuzi mbadala mzuri sana huu. Hongera mkuu. LAKINI, ulivyomalizia, umetupoteza zaidi. Kwanza, naamini kabisa kuwa hata wewe binafsi unajua kuwa sio uthubutu wa aina hiyo tunaouhitaji - uthubutu usio na elimu unaodharau taaluma, mantiki na sheria.

Pili unajua kuwa Magufuli anafaidi ujinga uliosimikwa nchini na TANU/CCM tangu awamu ya kwanza kwamba, baada ya yote, nchi itaendeshwa kwa “busara za rais”! Kwamba hakutakuwa na kuhoji wala kupinga maamuzi ya rais; kufanya hivyo ni uhaini! CCM waliung’ang’ania mfumo huo baada ya JKN kutoka madarakani wakitegemea ndio utakaowawezesha kutawala milele na kujichotea rasilimali za taifa bila “bugudha”.

Rais wa Tanzania ana madaraka binafsi juu ya taasisi zote za umma: serikali zote; mashirika ya umma; vyombo vya dola; tume ya uchaguzi; n.k. Maamuzi yake kwenye taasisi hizo ni ya mwisho. Akitaka pesa yoyote ni kiasi cha kumuagiza gavana wa BOT na/au paymaster general. Tena wao ndio watakaoandika maelezo ya justification.

Sasa, hapo inahitaji mtu anayeukwaa urais awe muungwana sana kufuata sheria na kujali haki za binadamu.

Msifu Magufuli kwa kuiona fursa kubwa aliyo nayo rais wa Tanzania na kuamua kuitumia bila simile! Nadhani hata waliojifikiri kuwa “mentors” wa Magufuli sasa jasho linawatoka. Huyu atavurugavuruga kila kitu mpaka waombe “poo”. Nilipoona akiwaswaga jamaa zangu serikalini kuhamia Dodoma na kuanza maisha kwenye magodauni na mapagala - na ikawezekana (hakukuwa na wa kukohoa) nikasema basi nchi imepatikana.

Sasa nasubiri kuona watakapoishia waliokuwa wakidai “CCM ina wenyewe” na “tuna hisa zetu CCM” huku wakimuona Magufuli kama wakuja tu (outsider). Wake up guys, Magufuli is now taking over CCM! Kwangu mimi hiyo ni hatua bora kabisa.

Labda itatusaidia kuwarejeshea akili Watanzania wenzetu hao waachane na tamaa za ki-fisi na kujiunga na juhudi za kuunda katiba mpya inayozingatia demokrasia makini na utawala bora unaoweka mbele haki za binadamu. Hii kutaka rais awe mungu ndio matokeo yake haya. Kila kukicha tunashuhudia watu wazima wakiadhiriwa hadharani kama hawana akili. HATUHITAJI UTHUBUTU WA KIJINGA NAMNA HII.
 
Yes tunahitaji Uthubutu kukataa kuburuzwa ili tunaowapa majukumu waanze kuheshimu kura na kodi zetu na kusimamia haki na kufuata sheria si kujifanyia wanalotakabkisa wana Uthubutu!
On that note, I say, THANK YOU Magufuli, kwa "Uthubutu". Hope this rubs off 'the right way' to the wananchi.

And THANK YOU, to the Rev. for finally making a clear definition of 'UTHUBUTU.

The only problem remaining now, is who will teach the "UTHUBUTU" lessons to the masses of Tanzanians who seem to have been in a trance, a spell of some type, hypnotized not to have these elements of 'UTHUBUTU'. Can Magufuli finally do this for us?
 
Rev.Kishoka, kama unaweza kufuatilia kwa makini unaweza kuona wachanagia wengi sana JF kwa sasa ni wapya, sio wale waliokuwepo tangu miaka 14 iliyopita wakati wana JFwanashambulia uozo serikalini. Wengi tulikuwa tunaomba atokee mtu ambaye atajilipua na kusema Tanzania kwanza, chama kwanza, ujinga mwisho.

Ukiangalia tangu serikali ya JPM ianza kazi we can see it is going for the jugular, at the same time inawapa kitu wananchi. Kuna uzi mmoja nimeweka kwenye jukwaa la Great Thinkers na kichwa "si kila mtanzania ni kichwa cha panzi", niliweka ule uzi nikikumbuka tumetoka wapi na malalamiko makuu. kweli JPM amethubutu.

CCM ya pre-Magufuli lilikuwa ni kama genge fulani lenye makundi ndani, watu walikwa hadi ushahidi hapa jinsi walivyokuwa wana-loot nchi...ingekuwa bora kama mijadala iliyokuwa hapa jamvini wakati Lowassa anatwambia uchumi wa Tanzania unapaa, na wakatu Dr Slaa anatwambia tunaibiwa. CCM ilikuwa imenunuliwa na ilikuwa ndio kinga kuu ya mafisadi, lakini CCM ya sasa ni chungu kwa mafisadi. Na inaonekana kuyafurumusha mafisadi kunahitaji moyo na umakini. Lakini badala ya kumsifu JPM kwa ku-dare ku-address root cause ya uozo ndani ya CCM na serikali, watu wanaanza kumdhahaki. What is it that we want? Tuendelee na ujinga ule ule just for the sake ya kuwafurahisha wanaojiita wenye chama? ...

It is absolutely ridiculous kumchukia JPM kwa kusema amekunyima ulaji, as if uongozi = ulaji. Kama ni kweli mtu anasema amemsaidia JPM kuingia madarakani halafu amemsahau, kweli hapa kuna tatizo, ina maana he is after something. Kwa hiyo licha ya upungufu uliopo kwenye serikali ya sasa, the least we can do ni kuwapa moyo na uungaji mkono.
 
Ukiangalia wote waliofanikiwa kimaisha, walicheza na neno "kuthubutu" umenena falsafa ya kweli , ubarikiwe
 
Uthubutu wa hovyohovyo unasaidia nini taifa ?

Fanya kitu kwa mipango ,busara na hekima siyo kukurupuka mpaka kuharibu nchi namba hii.

Uthubutu gani unaouongelea?

Kutoongeza mishahara kwa miaka minne? Kutopandisha madaraja watumishi kwa miaka minne? Kupora tilioni 1.5 ndio Uthubutu? Kununua kivuko kibovu? Kushindwa kuwalipa wastaafu mafao yao toka 2015 mpaka Leo ndio Uthubutu ?

Watu kutekwa, kuuawa, kufungwa kwenye viroba ndio Uthubutu? Kuteua vijana wa hovyohovyo kuwa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ndio Uthubutu? Kukandamiza demokrasia na haki za binadamu ndio Uthubutu? Kuwafungulia watu kesi za visasi za uhujumu uchumi feki ndio uthubutu?
Acha kulialia kuhusu mishahara acha kazi
 
Maghufuli atabaki kuwa icon kubwa sana, time will tell, ana mapungufu yake ila ni raisi wa aina yake ,hawa hawa wanaomlaumu ndo watakuwa wa kwanza kumkumbuka jamaa,
Sana tena sana,walimsema Sana mh kikwete lakini Leo ndo wakwanza kumsifia.nilichojifunza hata ungefanya Jambo zuri kiasi gani Bado wapo watakaoona hufai tu.
 
Lakini Uthubutu unaweza kuwa wa kufanya yalio mema na kufanya mambo mabaya.. msingi mkuu kujitambua ni je kila mmoja na uimara wa kufanya uthubutu wa yaliyomema? au uthubutu wetu ni wa mambo mabaya ikiwa ni pamoja na kuendeekeza UUMUU? je kama jamii inayapokeaje yale ya Uthubutu hasi ambayo ni mabaya? je jamii inakabiliani vipi na Uthubutu wa kuikandamiza na kuionea haki hata kuvunja sheria au matumizi mabaya ya madaraka na mamlaka?
Je jamii itathubutu kuamka na kukataa kudhulumiwa au kuruhusu Uthubutu wenye nia na matokeo mabaya?
 
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!

Uthubutu, ni uwezo wa kufanya mambo bila kuwa na kigugumizi au kujishuku. Ni kufanya mambo, kusimamia unaloliamini bila kujali au bila woga. Sasa kwa Magufuli ambaye tulijua akiwa waziri alikuwa ni mchapakazi mpaka kuitwa bulldozer, ilimaanisha alifanya mambo jinsi alivyoona ni sawa kwa nafasi yake na sasa kwa kupata Urais n kuwa Rais wa Jamhuri, basi Ari, Kasi na Nguvu zake za kuwa Bulldozer na uthubutu zimeongezeka maradufu.

Uthubutu si lazima tuutazame kwa matokeo chanya pekee, hata matokeo hasi yanaweza kutokea kutokana na mtu kuwa na uthubutu, kudhamiria na kufanya lile alilokusidia.

Rais Magufuli ametusaidia sana kutuonyesha kwa vitendo, na si semi, kauli au porojo kuwa kwenye nia pana njia.

Naam, kuna maamuzi mengi yaliyotokana na Uthubutu huu yameleta maswali mengi na hata matokeo ya "uthubutu" kuonekana kama hatua ambazo zilikosa weledi, busara, uhakika au hata hekima. Lakini cha msingi kwa andiko langu hili si kukosoa au kusifia mafanikio au kushindwa kwa maamuzi aliyoyafanya, la hasha... naangalia silika ya kibinadamu ya kuwa na uthubutu, Daring!

Nakumbuka miaka 10 ya Rais Kikwete, uongozi au utawala wake ulionekana umepwaya kwa kukosa Uthubuu wa ukali na kusimamia mambo yafanyike, bila kujali matokeo. Nakumbuka mgombea wa Urais 2015 Bwana Lowassa alinukuliwa mara kadhaa akisema Tanzania inahitaji mtu mwenye kufanya maamuzi magumu, na Watanzania ule u-soft soft wa awamu ya nne, ulitufanya tutake kupata mtu "Dikteta" kauli na nadharia ambazo kwa umoja wa Kitaifa bila hata chembe ya tofauti za kisiasa ai itikadi, ilikuwa ni "natural" kukubali uhitaji wa kuwa na Rais Mkali, Dikteta!

Magufuli kathibitisha katika uanadamu kuwa Uthubutu si jambo la kusadikika, bali li jambo la kweli, lina uhai na kila mtu akikusudia na kujiamini, anaweza kuwa na Uthubutu!

Nikiiangalia Tanzania ilipo leo hii, miaka 58 tangu tupate Uhuru ambapo bado tuko kwenye hatua za mwanzo za kujaribu kupiga vita Ujinga, Umasikini, Maradhi, Unyonge na Utegemezi (UUMUU)pamoja na kutamka kwa vinywa vyetu mahitaji ya maendeleo ya taifa kuwa ni Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora, sifa, hulka na wajihi wa kuwa na Uthubutu bado ni mchanga sana na ndio chimbuko la kukosa kujiamini, kuwa wanyonge na waoga kufanya maamuzi magumu.

Kuna dhana na falsafa inayosema fanya jambo, lisipozaa matunda chanya au uliyotegemea-matokeo hasi yanakupa fursa kurudia mchakato na kujifunza pale ulipokosea na kurudia jambo kwa ubora na umakini zaidi. Cha msingi ni kujiamini na kuwa na uthububu wa kufanya mambo.

Sasa kwa Tanzania yetu ya leo "Ya Magufuli" ya "MATAGA" na "CCM Mpya" utegemezi wa mwenye kujiamini na mwenye kuthubutu kumebakia kuegemea na kumtegemea mtu mmoja, Rais Magufuli. Wengine wote wamekaa kando wakishangilia na kusifia lakini hawana Uthubutu wa kwao wa kujitegemea na kwa nafsi zao bila kutegemea na kuzengea Uthubutu wa magufuli ambao sasa umeambatana na mamlaka na dhama kubwa kama Rais wa nchi.

Tumeshuhudia watendaji wa Serikali na Wanasiasa ambao wana majukumu ya kuongoza nchi, wakigeuka kuwa Wanyapara, wasiojiamini, wakitegemea sana UDola wa Kimamlaka na zaidi turufu yao kubwa ni kusema "maagizo kutoka juu" wakimaanisha ni maelekezo na maagizo ya Magufuli, wakikimbilia kuutegemea Uthubutu wa Magufuli kama ngao na nguzo.

Nasi wananchi ambao hatuna mamlaka au dhamana ya kiuongozi au madaraka, nasi tumekaa kando kwa unyonge au kuachia kila kitu kifanywe na kuamini na kutegemea "ah Magufuli ni kiboko".

Leo haki ya mwananchi inakanyagwa na kupuuzwa, tunakosa Uthubutu wa kudai haki na kusimama imara kukataa kuburuzwa. Ndio kuna hofu na mazingira ya kutishiana ambayo yanatufanya kukosa kujiamini, lakini kwa nini hatumtazami Magufuli yule aliyekuwa Waziri ambaye alisimama na kupata alichotaka na kudhamiria mpaka tukamsifia kwa ujenzi wa miundo mbinu Tanzania?

Nimesema awali, Uthubutu si lazima uzae matoke chanya (ambayo yanaweza kuwa ni mtazamo wa mtu, kikundi au wa aina moja au nyingine) au matendo yanayotikana na Uthubutu yapokelewe kwa mikono miwili na kila mtu. Lakini laiti kama kila mmoja wetu kwa miaka 58 tangu tupate Uhuru wetu tungekuwa na utashi, uimara, ujeuri, kujiamini na uthubutu hata kwa asilimia 50% a uthubutu wa Magufuli, si ajabu Tanzania ingekuwa mbali sana kwenye maendeleo yake ya uchumi, kupanuka na kukomaa kwa haki za watu na yote ambayo tunanung'unikia leo, si ajabu yasingekuwa manung'uniko au kero za kutukosesha raha.

Nikiangalia na kupima Uthubutu wa Magufuli, kuna mengi kafanya (kutenda si lazima kuwe ni sifa ya kufanikiwa jambo) kwa kuamua. Ama ni kutoa maagizo, kuamrisha na kusimamia kikafanyika bila kujali matokeo (consequences or final result) au kuangalia hisia za watu. Mfano, aliazimia kupanuliwa kwa barabara, kukafanyika ubomoaji ili kupisha upanuzi wa barabara hata njia ya reli ya SGR. Hakusubiri majadiliano ingawa yawezekana kukawa na gharama kubwa kwa maamuzi hayo hasa pale penye malalamiko ya fidia.

Akaamua kununua ndege kwa fedha taslimu, zimenunuliwa ndege 5 kwa mkupuo tena kwa fedha taslimu bila kuwa na ukiritimba ambao Serikali na ATCL walifanya kwa miaka 20 kabla ya Magufuli kuboresha au kuwezesha Shirika la ndege kuwa na ndege za kutosha (wengi mtakumbuka ndege za Mattaka). Akasitisha mazoea ya kusafirisafiri ya viongozi na watendaji wa Serikali bila kujali kama kulikuwa na umuhimu wa uwepo na uwakilishi wetu au la, lakini amri yake ilisikilizwa kwa kuwa alisema atatumbua. Leo tumeona Chato inajengwa kwa kasi kubwa; iwe ni maagizo, amri au watu "kujituma" kuhakikisha Chato inakuwa na hadhi kubwa na sasa inageuka kuwa kivutio cha biashara na utalii. Akasema kufanyike uhakiki wa vyeti, wa wafanyakazi wa Serikali, nayo yakatimia. Akasema lazima kila mtu apate stakabadhi akinunua bidhaa ili Serikali ipate mapato... leo kila mtu anahangaika kuwa na stakabadhi! Akasema lazima tuhamie Dodoma, iwe kumekamilika au la, watu wakahamia Dodoma, wengine ofisi ziko kwenye vibanda na wanakaa vyumba vya kupanga.. lakini Serikali imehamia Dodoma.

Sasa najiuliza, sisi kilitushinda nini miaka yote kufanya maamuzi kama haya?ni kigugumizi gani kilitushika kwa muda mrefu kufanya mambo na kuwa na uthubutu, bila kuwa na woga au kujiumauma? kwa nini tuliamini hatuna uwezo wa kufanya mambo kwa hiari lakini tunafanya sasa kwa kuamrishwa na ni sawa na kwamaba tunachapwa mijeledi, tunazinduka na kufanya?

Leo nina uhakika Magufuli akisema tunarasimisha Katiba ya Wananchi iliyotokana na Rasimu ya Warioba, litafanyika bila kupingwa au miguno. Sheria kadhaa na miswaada imepelekwa bungeni na "Chama tawala" ama kwa woga, unafiki au labda ukweli halisi kimepigia kura na kupitisha kila kilichopelekwa na Serikali ya awamu ya tano. Rais Magufuli leo akisema ni marufuku kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa, hakuna atakayebisha.

Sasa ni rahisi kusema yeye ana mamlaka makubwa na anatumia cheo chake, lakini ukweli unabakia kuwa anayafanya kutokana na Uthubutu, daring.. hata kama mara nyingine ni kiholela (reckless) au ni kishari (mercilessly), but he gets shit done regardless.

Je sisi wote tungeanza kujiamini na kuanza kuwa na uthubutu bila woga kufanya mambo tunayoamini ni haki yetu kikatiba, ni wajibu wetu kusimama kuyapigania. Iwe ni nyumbani, makazini, kwenye masuala ya kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiuzalishaji na kila jambo, uwe ni mfanyakazi, mwajiri, mfanyabiashara, mwanasiasa.. tukiwa wote na uthubutu, na tukafanya maamuzi kwa umakini lakini tukisimama imara kwa uthubutu, basi Tanzania ya Viwanda na Gurudumu letu la maendelo litapiga hatua kubwa na za haraka sana.

Lakini tukiendelea kwua Wategemezi wa magufuli, siku anaondoka tutarudi kule kule, kukwama matopeni na hata kuwa na mawazo potofu ambayo yanajengwa sasa hivi kusema tunahitaji Magufuli akae zaidi ya muda ulioko kwenye katiba.

Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu.

Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu!

TOO MUCH TO READ……!Summarize your story pse!
 
Kama kuna kitu cha wazi ambacho ni funzo kubwa kwetu Watanzania katika miaka minne hii ya Awamu ya Tano na "Utawala" (maksudi kabisa badala ya kutumia uongozi) wa Magufuli ni UTHUBUTU!

Namshukuru sana kwa kutuonyesha Uthubutu, tuungane, tusimame imara tufanye mambo kwa uthubutu kupata haki zetu na maedneleo ya kweli na endelevu. Ahsante Rais Magufuli kwa kutufundisha Uthubutu!
Katika maneno yote ya Kiswahili, sishangai kwamba umeamua kutumia neno uthubutu na naamini umefanya hivyo kwa makusudi maalumu kabisa…kuuzunguka mbuyu. Bila shaka umefanya hivyo katika muendelezo ule ule wa jitihada za kutaka kuficha sifa halisi ya mtu. Wenzetu wana usemi kwamba …you can put lipstick on a pig, but it's still a pig!

Hapana huu si uthubutu, huu ni udikteta, period. Sifa moja kuu ya uthubutu ni ujasiri na hiyo sifa dikteta hana kwa sababu ya woga. Dikteta hulazimisha wakati mwenye uthubutu (jasiri) hushawishi...dikteta kwa vitendo hulazimisha apendwe na ole wako umkatae, jasiri kwa matendo yake hushawishi kupendwa na hana kinyongo na wasiompenda.

Je ni uthubutu gani unaongelewa hapa? Uthubutu usiojali taratibu wala mwongozo? Usiohitaji mpango wala mkakati? Usiozingatia utu wala haki? Usioweka kwenye mizani faida au hasara? Usiotofautisha kati ya mwanga na giza? Usioheshimu sheria wala kanuni? Wenzetu wanao usemi kwamba … you can’t make a silk purse from a sow’s ear!

Hapana, huu si uthubutu ni ubabe, ukurupukaji na unyama…


 
Mbona mnatumia nguvu nyingi kumpamba huyu mwenyekiti wenu?!!!

Kiongozi gani hakuwa na zuri hata moja?!!!!
Umeona eh
Uthubutu wa nini?
Kama kuiba yeye ameiba zaidi
Wote ni walewale
Shida ya a WaTz ni nini?!
Kwa vile amewagusa Nape na January mko hapa mnampongeza
Ni mchezo mchafu Ni Ubabe na visasi


Wanachafuana hakuna mzuri hata mmoja

Yeye na watawala waliopita hakuna tofauti wote wezi period!
Kuna awamu ngumu kama hii? Nchi imejaa Hofu

Kukurupuka kwake kutamponza
Kibao kikigeuka mje hapa muwapongeze akina Nape
 
Watu wanaoshangaa ya Rais ni watu ambao hawaoni tuliko na tunakoelekea
Hata mtu akitaka kujenga ni lazima ajibane kweli kama hana pesa za mara moja

Itatuchukua mda kufika ila mwanzo mzuri na ipo siku matunda yataonekana

Uthubutu ndio umefanya watu waendelee ila tatizo la Nchi nyingi za Africa ni uvivu tu na kutokujali
 
IMG_20190707_230407_850.jpg
 
Back
Top Bottom