Uthubutu wa kufanya maamuzi magumu

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
333
Wakati mwingine mtu akisema jambo fulani la ukweli, wale wanaouswa na jambo hilo huja juu kumkebehi aliyetoa kauli husika. Hapa nataka kurejea hoja ya uongozi wa nchi hii kukosa uthubutu wa kufanya maamuzi magumu na sahihi au hata kama siyo sahihi lakini mtu awe amefanya maamuzi.

Siko hapa kupigia kampeni mtu yeyote, lakini Kauli iliyowahi kutolewa na EDO kwamba viongozi hawafanyi maamuzi magumu, na kisha akadhihakiwa, ndicho tunachokishuhudia leo, na ndicho tumekuwa tukishuhudia kila siku uchao. Suala la posho ya wabunge ni moja ya mambo ambayo kiongozi mkuu wa nchi ameshindwa kufanya maamuzi magumu, na kuwaambia watanzania kuwa jambo hili "nakubaliana nalo" au "sikubaliani nalo". Rais anatakiwa atoe uamuzi mmoja tu wa "ninaidhinisha" au "siidhinishi".

Kinachoneka, Rais anakwepa lawama ili isionekane kuwa yeye hahusiki na kuamua suala la posho wakati kwa mujibu wa katiba yeye ndiye mtu wa mwisho anayetakiwa kuidhinisha. Badala yake umebaki mchezo wa watawala au viongozi wengi serikalini ambao mtindo wao wa kuongoza ni kama ifuatavyo:

1. Spika napeleka mapendekezo ya nyongeza ya posho kwa ofisi ya waziri mkuu
2. Waziri mkuu anapeleka ushauri kwa Rais kikiwa na dokezo "mapendekezo yakubaliwe"
3. Rais anarudisha file kwa waziri mkuu kukiwa na dokezo "Please advise more on this, and consider the matter in a wise manner"
4. Waziri mkuu anarudisha file kwa spika kukiwa na dokezo "Please reconsider this matter wisely"
5. Spika anarudisha suala la posho kwa kamati ya uongozi ya Bunge
6. Spika na waziri mkuu wanasema Rais ameridhia (lakini hakuna mahali popote ambapo Rais amekubali kwa maandishi, maana suala hili haliwezi kutekelezwa mpaka katibu wa Bunge apate idhini ya maandishi "Decision instrument")

Spika-->PM--(ok)-->President--(Please advise)-->PM--(Please advise)--->Speaker---(Please advise)---->(Kamati ya Bunge)---(Usipoongeza posho tutakung'oa uspika maana tulishasema posho iongezwe)---->(Rais ameridhia)--->Ikulu--(Rais hajaridhia ongezeko la posho lakini nakubali kuna haja ya kuangalia upya nyongeza ya posho)?????????????????????????
 
kuna maneno kama haya nisiposaini wenzangu hawatanielewa, hata mkigoma mwisho wasiku mtakuja kwangu na mengine mengi tu..

huyu mkuu wa kaya msimtegemee kabisa katika maamuzi ya utata..
 
Back
Top Bottom