Katika awamu hii ya Tano Wakurugenzi wa Halmashauri huteuliwa na Mhe. Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Hii ni kinyume na awamu zilizopita ambapo uteuzi wa wakurugenzi Watendaji ulikasimiwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu.
Pamoja na nia nzuri ya Mhe. Rais ni vyema tukamshauri sisi wananchi wa nchi hii.
Jana tarehe 16 Julai, 2019 wakati Mhe. Rais akitoka kwenye mapumziko yake Chato kama kawaida yake lazima awasalimie wananchi kila anapopita.
Alipofika katika Mji wa Sengerema alisimama kuwasalimia wananchi na pale wananchi wakaanza kutoa kero zao mbele yake.
Kero nyingi zilielekezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na mjibu hoja alitakiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Pamoja na majibu mazuri ya Mkurugenzi Mtendaji, majibu yake hayakumridhisha Mhe. Rais.
Mkurugenzi hakuweza kufahamu Bajeti nzima ya Halmashauri yake 2019/20?.
Pili hakuweza kujua Makusanyo ya ndani ya Halmashauri yake. Alipoulizwa kuwa hapo mwanzo alikuwa anafanya wapi kazi, akajibu kuwa alikuwa mtumishi wa Benki.
Sasa napenda kumshauri Mhe. Rais kama mwananchi wa kawaida:- Uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri lazima utokane na UTUMISHI WA UMMA kwa maana kuwa Watumishi wanaoteuliwa lazima waufahamu vyema taratibu na kazi za Halmashauri.
Wawe wamekulia humo kiutumishi. Wapo watumishi wazuri sana ambao wako Halmashauri za Wilaya wenye uelewa na uzoefu wa muda mrefu kwenye Halmashauri wanaoweza kuteuliwa.
Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri walio na digrii za Phds, Masters, digirii ya kwanza na wanazijua vyema Halmashauri zetu na uzoefu wa muda mrefu hawa ndo wanafaa kuteuliwa.
Ni jambo la ajabu Mkurugenzi kutojua bajeti yake kwa mwaka ili hali yeye ndiye aliyeitayarisha.
Natumaini ushauri wangu utazingatiwa.