maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Hakuna jambo linalonifurahisha kama uteuzi unaofanywa na mheshimiwa Rais kuwateua vijana kushika nyadhifa za juu ktk wizara, mikoa na bila shaka kwenye uDC atajaza vijana watupu.
Nimemwona Dc wa Kinondoni ni kijana mdogo, Rc wake Makonda ni kijana, akiweka vijana Temeke, Ilala na Kigamboni nadhani wavivu wa wilaya hizo watakaoshindwa kwenda mchakamchaka wao watazikimbia wilaya hizo.
Kuna wakati vijana wa upinzani akina Mnyika, Zitto, Kafulila, Mdee, Sugu, Mkosamali, Lissu, Machali, Msigwa, Wenje, Lema n.k walionekana mastaa bungeni kila walipokuwa wakisimama kujadili jambo.
Vijana hao wachache walionekana kuliteka bunge kwa ujenzi wao wa hoja, lakini sasa naamini kuanzia bungeni na huku saiti Upinzani utaisoma namba.
Kwanza, huko Chadema kulikokuwa na upinzani wa nguvu, vijana wote machachari wameisharostishwa na uongozi wa Chadema tangu Lowassa ahamie huko ambaye kimya kimya lakini kwa ustadi mkubwa amekuwa akilipa kisasi kwa vijana wote waliomtangaza fisadi.
Imani yangu ni kwamba Rais akiicheza vema karata ya kuwapa nyadhifa za juu vijana wake, tutashuhudia Chadema ikiporomoka kwa kasi ingawa hili nalo si jambo jema sana.