Uteuzi wa kikwete ni fadhila au utumishi imepwaya, nina wasiwasi naye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa kikwete ni fadhila au utumishi imepwaya, nina wasiwasi naye

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kanga, May 8, 2012.

 1. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hivi JK na hawa wasaidizi kutoka katika taasisi binafsi na siyo utumishi wa umma yeye anawajuaje ufanisi wao na integrity yao kama siyo kutembea majina ya maswahiba na marafiki kwenye briefcase.
  Katika utawala wake ndio hii dhana ya uteuzi wa kutoka katika private firms imejijenga sana tofauti na awamu nyingine zilizopita na kwa kiasi kikubwa na ushikaji wa wanamtandao.Tazama punde baada ya kuchukua uraisi kitengo cha habari na mawasiliano alichukua wanahabari wanamtandao wote wakapewa nafasi ofisi ya Raisi yupo Salva Rweyemamu-mzee wa Kagera,Bi Mwingira aliyekuwepo wakati wa Mzee Mkapa akarudishwa mambo ya nje,wapo pia akina Premi Kibanga alikuwa BBC.Ofisi ya Waziri Mkuu yupo Ireni Bwire huyu alikuwa Mtanzania enzi hizo na Said Nkuba huyu alikuwa Uhuru akaenda Mwananchi kukaanga sumu ya kwamba DR.Salimu ndiye alihusika na mauji ya Mzee Karume na Ofisi ya Makamu wa Raisi yupo Kijana wa fujo UDSM Boniface Makene huyo alikuwa mwananchi na baadae Rai ya Rostam Aziz .
  Kwenye Ubalozi na Ujaji ndio kabisa wapo wazee wa IMMA Advocates-Mujulizi amepewa ujaji,Mwanaidi amepewa ubalozi na wengine ni jaji Dr Fauz alikuwa wakili wa kujitegemea na jaji mwingine ni Jungu alikuwa wakili wa kujitegemea kwenye ukuu wa Wilaya ndio usiseme.Miano ni mingi lakini kuna kitu anatufundisha siyo bure.
  Kwa mifano hii na wasiwasi na uteuzi wake kama unakidhi hasa vigezo vya utumishi wa umma na kama siyo mapenzi binafsi kama raisi kutunuku watu vyeo.
  Naamini katika uteuzi vyombo muhimu husika kama tume ya utumishi wa umma,mahakama,bunge nk.Hivyo katika kupitia majina hao hawawezi kupitikana kwenye orodha ya utumishi wa umma hivyo ni wazi rais ndio anawafanyia kazi vyombo vilivyoundwa kwa mujibu wa sheria kutafuta jina badala ya vyombo kupendekeza majina kwake na yeye kufanya uteuzi.
   
 2. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Umbea+majungu+fitna=UCHAWI
   
 3. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Jk huwa anateua watu njozini.Usishangae kesho mimi Maximilian Masanja nateuliwa kuwa msemaji wa baraza la mawaziri.
   
 4. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,290
  Likes Received: 1,444
  Trophy Points: 280
  Haya na mie aniote basi siku moja, maana ninachapa kazi mno kama, ninaamini nitaleta mabadiliko kwenye serikali yake.
   
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2012
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Jamani mlitaka atumie vigezo gani?atoe matangazo redioni na magazetini then afanyie watu interview? mwacheni afanye kazi na watu ambao anakua na amani nao na watakao kuwa watiifu kwake
   
 6. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mbona mtabiri na mfasiri wa nyota alishafariki !!!!
   
Loading...