Utetezi wa ACT-Tanzania ni dhaifu

Utetezi wa ACT-Tanzania ni dhaifu

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Gazeti la Tanzania Daima lilimuibua Edward Ngoyai Lowassa kama mfadhili mkuu wa ACT-Tanzania. Ikasemwa kuwa ni juhudi za Lowassa kuimega CHADEMA ili arahisishe kutimiza ndoto yake ya kuwa Rais wa nchi hii. Mtunza Hazina wa ACT-Tanzania akaibuka kujitetea kwa kukanusha kufadhiliwa na Lowassa. Pamoja na kanusho lake tamu kisiasa,akasahau kusimamia uwazi wa chama chake.Uwazi ulitaka kutaja waliochangia chama hicho zaidi ya milioni 74.Tena hawazidi watu 50! Kutowataja watu 50 muhimu ni kushindwa kujitetea. Ni muendelezo wa usanii wa kisiasa nchini.

Kauli ya Mtunza Hazina wa ACT-Tanzania ni hii:

Chama cha ACT-Tanzania hakina Mfadhili Mkuu
... 1. Katika toleo lake la siku ya Jumatano ya tarehe 30 Julai 2014 Gazeti la Tanzania Daima limechapisha habari zilizodai kuwa mwanasiasa moja maarufu hapa nchini ndiye mfadhili mkuu wa Chama cha ACT-Tanzania.

2. Kwa niaba ya uongozi wa ACT-Tanzania, na kwa nafasi yangu kama Mtunza Hazina na Mhasibu Mkuu wa ACT-Tanzania, napenda kuwataarifa wanachama na wapenzi wa chama na wananchi kwa ujumla kuwa taarifa hizi ni uzushi na uwongo wenye lengo la kuchafua taswira ya chama cha ACT-Tanzania. Napenda kuutaarifu umma kuwa moja ya misingi mikuu ya ACT-Tanzania ni uadilifu na uwazi. Kwa misingi hii, vyanzo vya mapato na matumizi ya ACT-Tanzania yapo wazi kwa mtanzania yeyote anayetaka kujua ukweli.

3. Tangu chama kianzishwe mwezi Januari mwaka huu, kimeshapokea na kutumia jumla ya shilingi 74, 857,000/= (milioni sabini na nne laki nane na elfu hamsini na saba) zilizochangwa na wanachama, wapenzi na wananchi wasiopungua 50 wanaouunga mkono misingi ya chama hiki. Taarifa ya kwanza ya fedha ya chama iliwasilishwa katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania katika mkutano uliofanyika Mjini Singida tarehe 25-26 Julai 2014. Kwa mtanzania yeyote ambaye angependa kuona orodha ya watu waliokichangia chama anakaribishwa kufika ofisi ya Makao Makuu iliyopo Ubungo National Housing mkabala na Hoteli ya Royal Njombe.

Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania

Peter Mwambuja, PGDA, CPA (T)
Mtunza Hazina na Mhasibu Mkuu wa ACT-Tanzania.
Imetolewa Jumatano 30 Julai 2014
 
Mleta mada ana maelezo dhaifu na mepesi sana, hayana uhalali wa kuwepo jukwaa hili
 
Hamuwezi kufanikiwa kuichafua a.c.t, mtahangaika na mwisho mtaharibikiwa
 
UNGEJIBU...WEKA HAYO MAJINA AU NIKUSAIDIE..LUWASA..ROSTAM ZITO endelea kutaja mku
 
Namimi narudi kusema bila kumung,unya maneno lowasa,rostam,nape,mwigulu na january makamba ni wafadhiri wakuu wa Act kigoma
 
Hamuwezi kufanikiwa kuichafua a.c.t, mtahangaika na mwisho mtaharibikiwa
Wewe ndio umekuwa wa kwanza kuianika act na udhaifu wake.

Au ulijisahau kabadilisha ID ?

Samamia ukweli kk achana na hivyo viposho vya kina zitto
 
Back
Top Bottom