CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,929
Lapokuwa gumu gogo, Shoka linapozidiwa,
Lipaswi pewa kisogo, Mbinu mpya hutakiwa,
Kwani gogo la mhogo, lishindwe kupasuliwa?
Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.
Msumeno ntatumia, gogo kulibanjuani,
Mbele kiushindilia, banzi walitakiani?
Nyuma kiurudishia, gogo lina gumu gani?
Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.
Shoka kazi yake kuni, Mpishi lampatia,
Kumletea jikoni, kuni za kumpikia,
Zikishapigwa juani, shoka inazipatia,
Seremala mwenye fani, shoka siyo la lazima.

Kuna gogo la muanga, njiani limeanguka

Waja mafundi kuchonga, kibanzi kutobanjika

Watu wavunjika nyonga, kwa kupanda na kushuka

Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

Waja wenye mbinu zao, hupanda wakadunguka

Waja na wavamiao, kwa papara na haraka

Wako pia waliao, gogo lipo lawacheka

Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

Letu sote gogo hili, kilitaka lakutaka

Afanyae hatambuli, mja huyo asumbuka

Thamani yake ni ghali, wala hili si dhihaka

Kula ajaye na shoka, katu hawi seremala

Hili gogo madhubuti, si rahisi kukatika

Tukishindwa tukaketi, bandu mwisho hubanduka

Tukikosa jizatiti, gogo litaja anguka

Kila ajaye na shoka, katu hawi seremala

Bandu humaliza gogo, hilo sheti kukumbuka

Tusijitie mikogo, kudharau kila shoka

Tusilikimbie zogo, pembeni jema kuweka