Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,301
- 33,920
Tarehe 7/7/2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania aliteua Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, miji na wilaya wapatao 185. Kati ya hao 120 walikuwa ni wapya wakati 65 wakiwa ni wa zamani. Wale waliokuwa wamefikia umri wa kustaafu walistaafu lakini wale waliokuwa hawajafikia umri wa kustaafu walielekezwa kuripoti kwa Maafisa Tawala wa mikoa waliyopo.
Swali langu kama taifa tumepata hasara kiasi gani kwa kuwa na watu wanaolipwa mshahara bila ya kuwa na kazi maalum ya kufanya? Lakini pia wapo vijana wengine wakiwa na miaka chini ya 40 wakiteuliwa kuwa Wakurugenzi jambo ambalo litaleta shida huko mbele ya safari.
Hawa vijana walioteuliwa kushika nafasi za Uafisa uandamizi (Senior Officer) maana yake wataanza mishahara yao kwenye ngazi hiyo na hakuna jinsi ya kuwashusha labda wawe wamefanya makosa makubwa sana ya kimaadili.
Maana yake kama wangeteuliwa watu ambao walikuwa kwenye utumishi wa umma kwa muda mrefu, ingekuwa ni nafuu kwa nchi kwani wasingekaa sana kwenye nafasi hizo au za juu yake. Kuna wengine hawajawahi hata kuwa wakuu wa idara wala vitengo lakini wamepewa nafasi hizo za uafisa uandamizi. Maana yake itachukua muda mrefu sana kuwalipa wakiwa kwenye nafasi hizo za uandamizi kuliko kama walioteuliwa wangekuwa ni watu ambao angalau wamedumu kwenye utumishi umma kwa muda mrefu na wanaelekea kustaafu.