Utengenezaji joto la kuku

tired

Senior Member
Feb 25, 2014
107
23
Wataalamu, Ninafuga kuku wa kienyeji. Mara baada ya kuku kutotolewa huwa nawachukua na kuwaifadhi tofauti na Mama yao. Mazingira ninayo ishi hakuna Umeme.

Naomba kujua ni njia gani bora naweza kuitumia ktk kuwatengezea vifaranga joto nyakati za Usiku.
 
Waweza tumia jiko la mkaa...likoleze then weka pemben au katikati ya chumba...

.
 
Good idea 'tired'
Ila hakikisha jiko limekolea kabisa ili kuzuia madhara ya carbonmoboxide inayotoka wakat Mkaa unakolea, kwani hupunguza kiasi cha oxygen kwenye banda na vifaranga hukosa nguvu au kufa kabisa.
.Njia nyingine Kama Kuku wako wengi unaweza kuwapangilia watakaoangua Karibu Karibu Kama wa4 basi unawaachia wa2 walee na wengine watage upya.
Vifaranga waliopulishana hadi siku 2 wanawezalelewa na Kuku m1 chakufanya ni Kuwaweka kwenye chumba kidogo chenye Giza kwa siku 2-3 ili ashindwe kutofautisha vifaranga wake na wa wengine. Baada ya hapo atawalea wote Kama wa kwake.
 
aksante sana
vipi kama nikitumia taa ya chemli nayo ina madhara yoyote?
 
Naona hipo njia moja tu ya Jiko la Mkaa. Ngoja nikajaribu njia hiyo hiyo
 
Na hilo jiko la mkaa jitahidi kuliweka ndani ya wavu wa waya ili vifaranga wasiungue maana ukiliacha hivyo hivyo joto linavyopungua wanalisogelea kabisa jiko.
 
Naona hipo njia moja tu ya Jiko la Mkaa. Ngoja nikajaribu njia hiyo hiyo
ungepata mtungi ndio rahisi zaidi kwa sababu haitakuhitaji kuamka mara kwa mara kwenda kuongeza mkaa. Mimi huwa naweka mkaa ndani ya mtungi na baada ya muda mtungi unapata joto na mkaa pia unaisha taratibu huku majivu yakizuia mkaa kuzima.
 
mtungi gani unasemea
 
Nashukuru sana kiongozi, nitaufanyia kazi ushauri huu
 
Nashukuru sana kiongozi, nitaufanyia kazi ushauri huu

Mimi nina box la ukubwa huu, upana na ulefu =100cm, kina = 110cm. Humo nahifadhi vifaranga wa siku mbili mpaka wiki tatu kwa utaratibu wa kumweka mama yao usiku na asubuhi namtupa nje na kuku mwingine akitotoa naongezea mpaka tofauti ya wiki moja anakuwa hawaelewi kwa kuwa hashindi nao.
Na kila nimletapo jioni namchunguza kama dk 5 kujiridhisha kama hawadonyoi, kisha naacha taa on mpaka walau saa 2 usiku, nazima naye anakumbatia watoto wote na kulala. Asubuhi namtoa mama na kuwasha taa mpaka saa 4 au 5 kutegemeana na hali ya hewa.

Zoezi hilo ni la wiki mbili(lazima), au tatu(kwa ajli ya kuwasogeza wale wadogo kama wapo). Baada ya hapo mama kuku harudi kwenye box tena.
 
Wataalamu, Ninafuga kuku wa kienyeji. Mara baada ya kuku kutotolewa huwa nawachukua na kuwaifadhi tofauti na Mama yao. Mazingira ninayo ishi hakuna Umeme.

Naomba kujua ni njia gani bora naweza kuitumia ktk kuwatengezea vifaranga joto nyakati za Usiku.

kuku mmoja anauwezo wa kulea vifaranga 25hadi30,hvyo unaweza ukatumia kuku mmoja kelea vifaranga kwa muda wa wiki tano kwa kuku chotara na wikisita kwa kuku wa kienyeji.Isipokuwa njia hii inahitaji usafi wa hali juu,kila wiki fanyia usafi na pulizia vrid usipo fanya hivyo nirahisi vimelea vya magonjwa kutoka kinyesi cha mama yao kuwapata vifaranga.Usiruhusu kuku kuzunguka nje na vifaranga tumia bluda au matenga mawili moja akae mama yao lingine utaweka maji na chakula cha vifaranga i.e starter.chakula cha mama yao tundika juu ya tenga lake vifaranga wasiweze kufikia.Tunatumia tenga kwsababu linamatobo makubwa hvyo inakua rahisi vifaranga wanapohsi baridi kukimbilia kwa mama yao pia tenga linazuia movement kwa mama yao.Kila la kheri!
 
tafuta jiko la mkaa wenye moto,tia sufuria juu ya jiko lenye moto unaowaka na kisha chukua vifaranga wako na watie ndani ya sufulia ambalo liko jikoni,acha kwa muda wa dakika 15,kisha ondoa,hapa vifaranga watakuwa na joto la kudumu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom