Utendaji wa nmb manonga shinyanga ni mmbovu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utendaji wa nmb manonga shinyanga ni mmbovu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pukudu, Oct 13, 2012.

 1. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli ni kwa muda Sasa utendaji wa Bank ya NMB MANONGA imekuwa ni MMBOVU tumelalamika kwa branch manager lakini hamna lolote ambalo linafanyiwa kazi... Baadhi ya malalamiko ni Kama ifuatavyo

  FOLENI.. Hili ni tatizo Sugu katika bank hii, kutokana na sababu wanazojua wao branch hii inahudumia watu kutoka wilaya ya Shinyanga mjini, Shinyanga vijijini, na Kishapu lakini CHA Kushangaza ni Kuwa madirisha ambayo yanakuwa na bank tellers ni mawili yakizidi sana ni matatu ni kawaida sana kusimama kwenye FOLENI kwa masaa mawili hadi matatu tena ikifika mchana huwa wanapokezana kwenda lunch so anabaki teller mmoja tu, huku WAFANYAKAZI wengine wakionekana wakirandaranda ndani tu. pia Sa nyingine nyie mko kwenye FOLENI wana acha kuwahudumia na kupokea slip zinazopitia kwa WAFANYAKAZI wengine kinyemela na kuwaacha nyie mkiwa kwenye FOLENI muda mrefu na ninasikia ili upate hiyo Huduma kuna amount unawaachia.

  2. POOR CUSTOMER CARE.. kwa kweli WAFANYAKAZI wa NMB MANONGA nahisi hakufundishwa kuhusu kuhudumia wateja Huduma ambazo ni haki ya mteja kuzipata ni kwa mbinde ukitaka kupata bank statement lazima wakuzungushe saana Mara utasikia network hamna Mara ooh tunatoa saa Tisa Mara subiri yani ni kero tupu, Mtu akifungua account inachukua hadi wiki 3 ndo upate account namba ili uweze kudeposit na account iwe active, halafu Sasa hadi upate kadi ni zaidi ya miezi 3, LUGHA wanayotumia WAFANYAKAZI ni ya dharau kashfa na kutojali YAANI ukiulizia kitu utakavyojibiwa utablow

  3. UZEMBE NA RUSHWA.. hili pia ni tatizo hii hutokea sana kwa account za makampuni, mashule na vikundi hasa pale mnapobadilisha signatories wanapokea form lakini hawabadilishi ktk computer ambao huleta usumbufu na ukiwaambia waangalie form mlizojaza wanasema sio kazi Yao YAANI kero tupu mnakuta picha na majina zimebadilika lakini sio sahihi, tatizo hili pia liko ktk uwe kaji wa cheque Kama hawakujui inachukua hadi siku nne ndo waifanyie kazi cheque yako Sa nyingine ni hadi uwafate ndo waishughulikie. Pia kwa WAFANYAKAZI wa serikali ambao mishahara Yao hupitia bank zingine wamekuwa wakipata usumbufu Kwan wamekuwa hawapeleki cheque wala majina ktk bank husika hadi ufuatilie ndo upate mshahara wako, hata ktk Suala la mikopo hata ka umekidhi vigezo vyote ili upate huo mkopo lazima ubembeleze na huchukua muda mrefu ka una haraka hadi uwahonge Maloan officer ndo utapata kwa haraka

  Kwa kweli kero ni Nyingi na wana boa Saaana hasa hasa kwa sisi watumiaji wa Huduma za bank ambao hatuna uwezo wa kutoa bakshish tunaumia na hatuna jinsi ya kutumia bank zingine yani tunalazimika kwa NAMNA au nyingine kutumia NMB nimetumia JF coz najua kupitia forum hii malalamiko yetu yatawafikia kirahisi . Hebu uongozi wa juu NMB. Walifanyie hili kazi na uchunguzi kwa kweli NMB MANONGA shy ni kero
   
 2. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,713
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  NMB NCHI NZIMA NDO HIVYO HIVYO...Si wateja rukuki,!
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  wiseboy shinyanga wamezidi yani muda wa kazi unawakuta wafanyakazi wako lunch wanapiga story huku wameacha foleni, hivi cheque book inachukua miezi sita kupata? Au ndio utaratibu wa NMB, HATA kufungua account nisubir wiki nne? Statement kupata pia nihustle? data pia kutunza ni mfumo wa bank? Eti hata kubadilsha signatories ni issue, teller wawili kuhudumia watu mia na zaidi ni sawa ilhali wafanyakaz wengine wako tu huko ndani wanasubir slip za magendo wapate chochote? nmb shy kuna uzembe uliotukuka
   
 4. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  hayo yanapatikana kote kwenye matawi ya nmb mikoa, sijui kuwe na benki 2 za makabwela!
   
Loading...