UTEMI na UFISADI Kuimaliza CCM

Wafanyakazi wa New Habari corporation wote mtawatambuwa kipindi hiki. hata gazeti la mtanzania liangalieni mtajuwa kwamba hawa watu maslahi yao yameshakwisha ccm, sasa wanaona aibu walisahau mwisho wa ubaya ni aibu.

..One time i agree with Matola, haupo mbali sana na ukweli.
 
Habari WanaJF

Ni masikitiko yangu kuwa wazima, lakini napenda kutoa dukuduku zangu juu ya chama changu ccm
kwa kuendeleza utemi nakutosamini wanachama wake, wengi wa wanachama wamekikimbia kwa sababu ya utemi na ufisadi.

Kamati kuu imefanya maamuzi yake na kumchagua nape ambaye ni mchanga katika siasa za tanzania na kuishia kuropoka kila wakati, mambo mengine sio ya kuropoka lakini yeye anatumia jukwaa kuropoka, Je kamati kuu ilikosa mtu makini wa kubeba jahazi? kamati mpya imefanya ziara mikoa mingi lakini muitikio wake ni mdogo vijana wote wamekimbia. Je hapa manajenga chama gani? Kama wazee ndo wamebaki CCM

sisi wanachama wadogo tunauzunika sana mana tulikuwa tunafikiri tumepata nafuu ccm inajivua gamba lakini sasa ni kinyume, wameshidwa kuwafukuza mafisadi maana wanawajua kwa majina. Wanachama tunakililia chama chetu

Rais tunaomba uwasikilize wanachama wako chama kinaangamia, hakina mvuto tena kwa sura ya watanzania

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki CCM

...jk, nashawishika kukujibu na kukushauri. kwanza, ukiwa kama kijana inapendeza kuona kuwa umebaini nini hasa kinachotokea katika hicho chama. ni vyema siku zote vijana kama ninyi mkawa na mtazamo ulio wazi juu ya masuala mbalimbali ili muweze kukisaidia chama chenu, na kusikiliza ushauri wa wenzenu, ndani na nje ya chama.

...pili, lazima mtambue kwamba hao mnaowaita mafisadi wakuu ndio uhai wa chama chenu kwasasa, msinyee kambi. kila mtu mwenye uelewa wa kawaida na anayefuatilia siasa nchini anafahamu mchango wao mkubwa kwenye chama, haijalishi ulihusisha ufisadi au la. sasa, mlitakiwa kuwatumikia wananchi na si kujisahau na kuvimbiwa matumbo, mkingojea mlo mwingine (uchaguzi mkuu ujao) kwa hamu na fujo. huwezi kula bila kufanya kazi, at least not for long!

...tatu, inabidi muelewe kuwa mapambano dhidi ya ufisadi si ya siku moja na ya kutangaza majukwaani. mnaaibika, kwani kazi haifanywi kwa maneno bali matendo. mnatakiwa kusahau yaliyopita, muweke misingi imara ya uwajibikaji katika chama na kuisimamia, hatimae isambae hadi kwenye serikali mnayoitawala. pia, mwanze kuwaondoa wababaishaji kwenye utendaji wa kila siku wa chama, mkianzia na huyo nape wenu. he is a liability!

...nne, kama kweli wewe ni kijana wa ccm, basi tafuta wenzako wenye mtazamo sawa na wewe mwanzishe mapinduzi kwenye chama chenu. ila nionye, si kazi rahisi na inahitaji wito na moyo mgumu.

...tano, itakuwa vizuri kama vijana wenzako watajitokeza kama wewe na kuwa wakweli ili muungane katika kubadilisha hali katika chama chenu. otherwise, tunategemea kuwaona katika nafasi ya upinzani mwaka 2016, inshaallah!
 
Nape si yule mtoto wa Marehemu brigedia Mosses Nnauye?

Nape amesoma wapi au ni shule za ku unga unga?

Akitoka baba mwana anaingia, hata kama hana upeo

Badala ya kushughulikia umasikini wa watanzania, wanaangalia mambo binafsi ya watu

Yaani mpaka Harusi unachangiwa na Jeetu Patel, kwani huwezi kuoa mpaka uoleshwe?
 
Back
Top Bottom