chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 15,226
- 25,978
MOJA: iandaliwe charge(mashitaka),kwa muktadha wa hawa wanaodaiwa wana vyeti feki,basi mamlaka yao ya nidhamu,baada ya kuchunguza na kuona wanatuhumiwa,basi wangeandaa hati ya mashtaka dhidi yake na kumkabidhi
Katika tukio la jana, bwana mkubwa alikabidhiwa ripoti na akawafukuza kazi mara moja bila kuwaandalia mashtaka ya kiutumishi(sio ya kimahakama),
MBILI: wahusika,kwa mujibu wa sheria hiyo walitakiwa wapewe haki ya kusikilizwa baada ya kushtakiwa kiutumishi,hii ni haki ya kujitetea na kuelezea upande wao wa story ......lakini kwenye hili,hawajapata hii fursa,fursa hii huja baada ya kukabidhiwa hati ya mashitaka,na ushahidi wao,na wewe unaambiwa u-show cause kwa nini sasa usifukuzwe kazi kwa mujibu wa ushahidi unaokutuhumu kwamba umeghushi vyeti
TATU: Inquiry,ambayo sasa ndio uendeshaji wa kesi yenyewe,huyu kamuhoji yule na mengineyo
Hapa naongelea "mahakama zilizo ndani ya utumishi wa umma" ambazo ngazi yake ya mwisho ya rufaa ni Rais/Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais,tatizo linakuja pale Mamlaka ya mwisho ya rufaa,Taasisi ya urais inapoonekana tayari imefanya maamuzi kabla ya mamlaka za chini hazijakaa na kuandaa utaratibu wa mashtaka!
Ni sawa na kumsikia jaji anakutaja kwamba wewe ni "mwizi na jambazi" na unajua kesho unaenda katika mahakama yake ili akusikilize
Kitu ambacho angefanya bwana mkubwa ni kuzitaka mamlaka zichukue hatua kwa mujibu wa sheria,mara moja taratibu hizi zingekuwa activated na maafisa utumishi kwa kufungua mashtaka rasmi,na mwanasheria mkuu wa serikali naye kuitisha jopo lake