SoC02 Utawala wa nchi yangu Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Seifmasoud54

New Member
Sep 8, 2022
1
0
"Tanzania Tanzania Nakupenda kwa moyo wote,
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana......."

Tanzania nchi iliyopo ndani ya bara la Afrika katika ukanda wa Afrika Mashariki inayoundwa na mikoa thelathini na moja ikiwa na kilometa za mraba 947,303 na watu wanaokadiliwa kufikia mamia milioni kwa mwaka 2022. Ikiwa mji mkuu wake ni Dodoma na jiji kubwa zaidi ni Dar es salaam.

Nchi iliyo barikiwa vivutio vya utalii, mbuga za wanyama na masalia ya maisha ya binadamu wa kale, nchi iliyo pambwa kwa madini ya kila aina na mengine yasiyo patikana popote ulimwenguni yanapatikana Tanzania, nchi yenye mabonde na milima yenye sifa na majina makubwa kama mlima kilimanjaro unaopatikana kaskazini mwa nchi ya Tanzania, nchi iliyobarikiwa gesi asilia bila kusahau madini hatari yenye thamani yaani nyuklia.

Nchi iliyo zungukwa na bahari ya india ikiwa na bandari zake kubwa tatu tangu enzi za historia, nchi yenye watu weusi wakarimu wacha Mungu, watulivu ,wachangamfu, wacheshi na wanyenyekevu ,bila kuwasahau wachapakazi na wazalendo , nchi inayo undwa kwa bara na visiwa.
Nukuu fupi ya taswira ya nchii

UTANGULIZI

Mwanzo 1:28 *
"Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”..."
Nukuu toka kitabu cha biblia

Utawala ni muongozo tulio pokea toka kwa Mwenyezi Mungu mlezi wa kila vilivyomo ndani ya ulimwengu toka enzi za kuanzishwa ulimwengu. Wapo walo sema uongozi ni tunu, wengine wakasema ni wito, na wengine wakasema ni kipawa/talanta. Lakini mimi leo naandika nikinukuu kutoka katika kitabu cha mwanzo 1:28 kuwa uongozi ni agizo toka kwa Mungu.

Kwanini utawala?

Msingi wa maendeleo na mafanikio yoyote katika maisha ya binadamu yanaanzia katika uongozi katika ngazi zote kujitegemea, familia, jamii, mkoa mpaka taifa. Rasimali yoyote kwenye maisha inahitaji usimamizi sahihi na uongozi wenye tija ili kuleta manufaa katika mazingira husika.

Karne ya leo uongozi umemezwa na demokasia, kumekuwa na watu wanao jiita wanasiasa, limekuja wimbi kubwa la vita vinavyo vunja amani upendo na uzalendo kwa vitendo vya ukatili kama vifo vya viongozi wasio na hatia na wengine kupewa vitisho, utekaji na kunyimwa uhuru wa kujielezea .

Utawala umekuwa sahani ya chakula cha mafisadi kupitia demokasia, angali watawaliwa wamekuwa wakilia kila siku kwa kukosa suluhu ya matatizo yanayo kumba jamii kila kukichaa, tena demekosia imekuwa nafasi ya kutajirika ukiachia mbali kafara na imani za giza, kwani mwanasiasa amekuwa tajiri mkubwa nchini kuliko hata mfanyabiashira hapa nchini.

Je, demokasia ndo adui wa maendeleo ya Tanzania?

Nukuu toka darasani; swali pendwa la watunzi wa mitihani mashuleni kwa vijana,

"Tanzania ni nchi tajiri wa rasimali nyingi sana , lakini watanzania ni watu wenye maisha duni, na uchumi wa nchi bado uko chini."fafanua.

Ni kweli ni swali jepesi sana kwa mwanafunzi lakini ni swali zito kwa viongozi, ni viongozi wachache walijaribu kulijibu hilo swali lakini majibu yao hayakufika mbali yakageuzwa na wale walio karibu yao, tafsiri yake kwa akili ya kawaida, kwa kutumia misemo ni kuwa ,"mchawi wako ni wewe mwenyewe"

Demokasia ni mfumo huru, wenye kutumia haki usawa na maono katika kutekeleza majukumu na uongozi kwa uwazi ,ukweli na amani. Licha yakuwa walio ileta demokasia waliitumia kwa manufaa ya kutunyonya na kutukandamiza (makoloni) licha ya viongozi wetu waandamizi wa kwanza hayati MWL. JULIUS NYERERE kujaribu kulipinga hilo na kupendekeza siasa ya ujamaa na kujitegemea ambayo nayo ilikuwa ngumu kwetu kwani ndo kwaanza tulikuwa tunaanza kutaka kuwa nchi huru ya kujitegemea.

Kijiti hakikuishia njiani mpaka pale demokasia ya kibepali ilivyo changanya katika mfumo wa vyama vingi mnamo mwaka 1992, ambapo sura halisi ya demokasia na siasa vili dhihirika katika nchi ya Tanzania mpaka hivi leo.

Hivi ni kweli majibu hatuna?..ni nani wakutujibia na kutuamlia?

Ni yupi kiongozi bora?

Ni kweli Tanzania haiwezi kuwa nchi yenye uchumi wa juu zaidi barani Afrika? Na je , ni kwanini?

Ni kweli kuwa siasa na demokasia ndo adui mkubwa wa maendeleo ndani ya nchi ya Tanzania? Je , ni nini chanzo ?

Ni kwanini mwananchi wa kawaida ndo mhanga mkubwa wa maamuzi ya kiuchumi yanayo fanywa na viongozi wake?

Je, ni kweli ukatili, vitisho vita vya wenyewe kwa wenyewe vita fika kikomi ndani ya demokasia ya Tanzania?

Ni lini Tanzania itasifika tena kuwa na kiongozi mzuri ambaye atachukiwa na walowezi na kupendwa na wanyonge?

Ni kwanini leo tunalaumu uongozi nchini? Je , hawa viongozi wetu waleo sindio kaka zetu na dada zetu jana na juzi?

Leo ni nani wa kulaumiwa ? Viongozi wakitanzania? Kwani uzalendo aliufundisha nani? Mbona hakuna anae jali kuwa sisi ndugu wa kitanzania? Mwingine anatembelea gari mwingine analala barabarani, ni nani wa kulaumiwa? Wakati waziri anatembelea msafara wa magari, kipindi bodaboda wanalia bei ghali mafuta, familia zao hakuna anaezijali wanasubiri takwimu za ndoa kuvunjika kwa mwezi waposti kwenye vyombo vya habari, na hii ndo Tanzania
.
JICHO LANGU MTANZANIA

Inawezekana Tanzania kuandika historia zaidi ya zilizo andikwa katika majarida ya uongozi barani Afrika, kama msingi utaanzia chini katika kuandaa na kuwalea viongozi wazalendo kutoka hali za chini tena hasa wale wanao toka katika familia peke(yatima) kuwapa nafasi ya kuelewa kuwa sisi sote ni ndugu. Kuwapa urithi wale wanao stahiki na si wale ambao wana kidhi kwa kutengenezewa mazingira ya upekee ambao wengine hawakuwa nayo.

Inawezekana Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kuchochea uzalendo na umoja kupitia viongozi mashupavu na kuifanya Tanzania na watanzania kuishi maisha yenye hadhi na kupiga vita umaskini nchini kupitia usimamizi mzuri wa utajiri wa rasimali zilizopo nchini kwa iwekezaji ulo na tija na wenyewe manufaa makubwa kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Inawezekana Tanzania ikawa nchi ya uwazi ukweli na amani kama serikali itamjali mwanachi wa chini katika kila hatua ya maendeleo na mikakati yake ya utekelezaji wa majukumu yake nchini kulijenga taifa la Tanzania kwa kuhamasisha vijana kujitoa kwani wao ndo warithi wa taifa hili.

Inawezekana Tanzania kuwa nchi inayo amini na kuthamini zaidi mchango wa kijana na kuwawezesha wale wenye kujitoa na wenye vipawa kama wigo wa kuchochea kukua kwa uchumi katika ngazi ya mwananchi mmoja mmoja na hata jamii kiujumla na hili linawezekana kama vijana wenye taaluma kupewa kipaumbele katika nafasi za uongozi zinazo husiana na taaluma zao.

Inawezekana Tanzania kuwa nchi yenye demokasia ya mfano kwa kutengeneza viongozi mashughuli viongozi waadilifu viongozi wazalendo viongozi wanajali maslahi na kuheshimu siasa na kutekeleza majukumu yao ipasavyo, kuwa viongozi wanaelewa zaidi hali za wananchi wao kuliko hali zao, kupitia demokasia ya uwazi ukweli na amani.

TANZIA

Bila shaka watanzania tunatambua mchango wa viongozi tulio tamani kuwa nao leo lakini Mungu alikwisha kamilisha kusudi la kazi yake kwenye maisha yao, wametujengea nchi yetu kwa amani kwa mazuri pia papo walipo kosea na Mwenyezi Mungu uwahurumie na awasemehe.
Heshima kwa viongozi wote walio tangalia mbele za haki
Kiti cha Uraisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mwenyezi Mungu awahifadhi.

KWETU WATANZANIA

Wakati umefika nchi yetu kuijenga, hakuna cha kuficha tunajua tulipo teleza , kusema peke ake, haina maana yoyote zaidi ya kuhamasisha vurugu na kuvunja amani, ni wajibu wa kila mtanzania kuwa mzalendo kuwa mkweli na muwazi kwaajili ya maendeleo ya nchi yake. Maana yake kiongozi hayupo kwaajili ya kufanya kile awezalo tu, bali kila mtanzania anafasi na mchango kwa kiongozi wake kuibadilisha Tanzania ya sasa kuwa Tanzania ile tunayo itamani.

HITIMISHO

Kila palipo na maendeleo na ustawi wenye manufaa na wakuvutia basi kulikuwepo na uongozi mzuri ulio simamiwa kwa haki usawi na kuleta matunda mazuri kwa jamii nzima mpaka vizazi na vizazi kujivunia.

Pia palipo kuwa na mmomonyoko wa maendeleo ,ubadhilifu pamoja na udanganyifu katika matumizi ya rasimali kulikuwepo na uongozi. Iheshimike na ieleweke kuwa uongozi ndio nguzo ya taswira ya mafanikio katika jamii yoyote ile.

Kuhitimisha, kila safari ya mafanikio inakipindi kigumu ambacho kinahitaji mshikamano, uvumilivu na uzalendo.

*MUNGU IBARIKI TANZANI
MUNGU WABARIKI VIONGOZI WA TANZANIA
MUNGU TUBARIKI WATANZANIA*
 
Back
Top Bottom