Utawala bora mashakani

Utawala bora mashakani

pepopunda

Member
Joined
Sep 16, 2013
Posts
13
Reaction score
7
Wana Jamii jana nilisikia kilio cha wakazi wa mkoa wa Kigoma wakilalamika kwamba wapo baadhi yao waliokamatwa kwa hisia kwamba sio raia wa Tanzania.Watu hawa walikamatwa vijijini na kupelekwa Kigoma mjini na walikaa chini ya ulinzi wakati wakifanyiwa mahojiano ili kutambua uraia wao.Jambo la kusikitisha ni kuwa wale ambao walithibitika kuwa ni raia wa Tanzania waliachiliwa huru lakini hawakupata msaada wowote wa kuwarejesha makwao.Ninachojiuliza hapa je,walichofanyiwa na serikali yao ni sahihi?Wote tunajua hali ngumu ya maisha ya wenzetu waishio vijijini.Serikali hii inajali raia wake?
 
Back
Top Bottom