SoC03 Utawala Bora Kwa Elimu

Stories of Change - 2023 Competition

allan_gobe_tz

New Member
May 31, 2023
3
3
Yapata kama miaka mitano hapo nyuma baada ya Kijana mmoja jasiri, mkakamavu, shupavu na mwenye bidii katika maisha ya Kila siku aliyejulikana Kwa jina la Kunze kupitia changamoto ya ubaguzi wa kitabaka kwani alikuwa Mwenyeji wa Bara. kijana huyo baada ya kufikia hatua ya masomo ya elimu ya juu akaona ni vema masomo yake Kwa vitendo kufanyia katika kisiwa jirani kwani aliona ni nchi moja na yenye upendo na amana.

Hakusita kufanya hivo baada ya kuweza kukubaliwa na kujiunga na masomo Kwa vitendo(Field practice) nchini humo kisiwani alisafiri mpaka kuelekea kisiwani nchi yenye eneo la mraba maili 200 kuizunguka yote ni nchi ndogo lakini yanye mambo makubwa Sana kwani inajali watu wake pamoja na dini yake. Kijana huyo Kunze hakuwa na lakufanya kwani alijikuta mpweke Kwa kuwa dini yake haikwendana na wakazi wake piah na lakini hakukata tamaa Kwa Hilo. Baada ya siku kadhaa kuanza mafunzo yake Kwa vitendo katika Banki aliwajibika ipasavo kwani Bado alitakiwa kuludisha matokeo mazuri Kwa ndugu zake wajivunie walichokipanda.

Siku moja alionekana Kunze katika stend ya mabasi ya daladala Duka kubwa akiwa na msongamano wa watoto wa skuli za misingi na sekondari kuelekea kazini M/Kwerekwe, mara ghafla basi la kwanza likapita likiwa limejaa nakuanza kugombania pamoja na watoto wa shule hakuona sawa akaacha kwanza wanafunzi wafike shuleni na kusubiri gari la pili. Haikuwa mda mfupi mpaka anafika ofisini Kwa maana ya foleni njiani pamoja na askali wa barabarani kusimamisha magari Kwa mda mrefu Kwa sababu ya kiusalama zaidi.

Hatimae anafika mpk Ofisini, moja Kwa moja mpaka office ya manager wa Bank aliyejulikana kama Boss Ameir Kheir baada ya salama ilionekana Kunze hayupo sawa ki psycholojia kwani alikuwa mtu wa mawazo mengi Sana, Boss alimuuliza, Kunze uko saw?

Mbona unaonekana mtu mwenye mawazo Sana. Kunze alista kidogo na kumjibu Boss wake, nkweli Boss Wangu changamoto hasa ni Hali ya kiuchumi siyo nzuri tunakuja field wanafunzi wengi lakini tuna changamoto hasa za kiuchumi hususani nauli za Kila siku hatuna na ukilinganisha na serikali ya Sasa suala la mikopo imelipuuzia Sana pesa za kufanyia field practice hawatoi tunapata changamoto kweli mpaka wengine kuishia njiani hawamalizi mafunzo Yao, pia na Hali ya usafiri shida kutokana tunatoka mbali. Kunze aliongea hayo Kwa uchungu kwani ilikuwa Si Hali ya kufurahisha.

Boss alimtuliza kijana huyo Kwani alimtia moyo kuwa akubaliane na mabadiliko ya nchi zetu za kiafrika kwani uwajibikaji na utawala Bora umebakia kuwa ni hadithi za abunwansi, alimpa moyo nakusema jitahidi kuwajibika katika majukumu Yako ya kazi kwaani Ipo sku utafankiwa yote yatapita. Boss alimsikitia kijana mdogo huyo Kwani alionyesha Hali ya hudhuni mpaka kutokwa machozi, alimuaga na kumhaidi baada ya kazi aende akampatie pesa ya nauli ya kuludia nyumbani.

Kunze alishukuru Sana na kuelekea katika majukumu ya Kila siku, baada ya kufika mlangoni mwa Office ghafla na kusikia wafanyakazi wakilaumu kuwa wanafunzi Hawa wa field Bora wamalize waondoke kwani wanawaharibia kazi zao, ndipo KUNZE alipo kumbuka juzi alipo shindwa kutumia Excel system za account kwani Programu hiyo chuoni kwao ilitolewa Kwa malipo na hakuwa na kujiweza kiuchumi.

Yote hakujali baada ya kuskia hayo kwani yeye aliendelea kujituma katika majukumu yake ya Kila sku huku Madamu Bim kashikria kikombe Cha chai na chapati pamoja na Madamu Sherry akiwa anakula chips na nyama, Kunze mate yalimtoka kwani alikuwa na njaa Kwa maana ya Jana alilala bila ya kula haikuwa na namna aliwajibika kazini kwani anaamini ipo sku atapata ajira yake.

Chakula chake kilichomfaa yeye ni mabaki ya mandazi pamoja na maji ya kawaida alipitia mazingra magumu lakini hakujali. Baada ya mda wa kufka ipatapo saa 10 alasiri tayari Sasa kurudi nyumbani akiangalia mfukoni nauli Hana lakini akakumbuka kuwa Boss wake alimhaidi kumpatia baada ya kuchukua tayari na kuelekea nyumbani.

Baada ya kufika nyumbani hakuwa sawa kiafya akaona ngoja aende hospitalini kuweza kupata dawa hata za kupunguza maumivu ya kichwa, kama ulivo utawala Bora wa nchi za kiafrika alifika hospital na kukuta foleni ya watu wapatao kama 20 akabaki kuwa mwisho na kusubiria huduma, ikapita kama dakika kadhaa mara akapita Baba mmoja alieonekana mtu mwenye hadhi yake na pesa akapita na kuingia chumba Cha Doctor, watu tulistajaabu kwaani haikuwa haki Kwa Hali ya kawaida, Kunze Kwa jeuri la elimu alipita mbele na yeye aweze kuingia ndani alifukuzwa nje na kuambiwa asubirie njee asijifanye anaharaka Sana au anaumwa Sanaa akauliza huyo aliepita mbele yetu wakati katukuta anaharaka Sana?

Kunze aliuliza Kwa ujasiri mkubwa Sanaa, alichojibiwa ni kwamba ajilinganishe yeye na wewe hapo nani atangulie kuingia, sikuwa na lakusema kwani sikuweza kujua sheria ya kupambana Wala na kuhoji Zaidi ya pale nlirudi Kwa hasira na kuweza kughairi kusubiria huduma kwani nliona Hamna utawala Bora Kwa wananchi hususani wanyonge nchi ilijinufaisha na kujali watu wa hadhi ya juu na kusahau wananchi wanyonge. Hakuona ajabu Kwani Bado alitumia uzalendo wake kwani Bado nchi Moja Kwa hivo aliomba mungu sku Moja yataisha.
 
Back
Top Bottom