Utaumia sana, utateseka sana kama furaha yako inategemea mpenzi wako anavyoku treat

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Katika ulimwengu wa mahusiano fanya ufanyavyo ila hakikisha furaha ya moyo haitokani na mpenzi wako anavyo kutreat bali furaha yako ya moyo itokane na jambo lingine .

Kuna wakati yes unatamani usikie maneno mazuli kutoka kwa mpenzi lakini huyasikiii,

Kuna wakati unatamani kuona mpenzi wako lakini hafanyi hivyo

Kuna wakati ukiamka asubuhi unatamani ukutane na neno zuli toka kwa mpenzi wako akikuamsha na neno good morning love lakini unakutana neno good morning john inakuwaje

Kama wewe ni mtu wa aina hii basi tegemea kuishi kwa shida sana na maumivu makali mnoo
 
Acha mapenzi yatuue tu..
Hizo motivation quotes ni sababu umeachwa au penzi lako lina migogoro.. acha sisi tufaidi kwa sasa siku tukipigwa na kitu kizito tutakuunga mkono..

Shemeji yako anakusalimia
 
Eleza vizuri kwanza kilichokusibu tukusaidie! Don't speak indirect way.
Aisee nilikuwa katika mahusiano na binti fulani ivi huyu binti off course nilikuwa mtu wa aina hiyo lakini sasa

Ilifika hatua niliona why haya mahusiano yananiumiza hivi tofauti na matarajio yangu nilichoamua kukifanya ni kupambana kumtoa binti moyoni mwangu baada ya hapo sasa.

Binti kuna muda aligundua kuna kitu hakipo sawa ikambidi aanze kufunguka eti siku hizi nimebadilika
Kumbe yeye ndo kabadilika

Alivyoona maji yapo shingoni akaniomba tuanza upyaaa
 
Aisee nilikuwa katika mahusiano na binti fulani ivi huyu binti off course nilikuwa mtu wa aina hiyo lakini sasa

Ilifika hatua niliona why haya mahusiano yananiumiza hivi tofauti na matarajio yangu nilichoamua kukifanya ni kupambana kumtoa binti moyoni mwangu baada ya hapo sasa
Binti kuna muda aligundua kuna kitu hakipo sawa ikambidi aanze kufunguka eti siku hizi nimebadilika
Kumbe yeye ndo kabadilika

Alivyoona maji yapo shingoni akaniomba tuanza upyaaa
Sasa hapo kwenye kuanza upya ndiyo unapo kuja kupigwa mazima na kulia kilio cha mbwa koko bwiiiiii.
 
Sasa hapo kwenye kuanza upya ndiyo unapo kuja kupigwa mazima na kulia kilio cha mbwa koko bwiiiiii.
Baada ya kuona penzi limeanza kudodorora siku baada siku ndipo kinapokuja kipengele cha tuanze upyaaa

Na hapo ndipo unaanza kujiuliza moyoni inawezekana tupo wawili baada ya kuona mambo yameharibika upande ule mwingine basi mtu anapambana aweze kurekebisha ukuu au unakuta baaada ya kuona huku ameshaharibu na kule hakuna uhakika basi inabidi huku apambane apajenge kwanza
 
Hakuna upo peke yko mademu ndivyo walivyo ukiwapa attention wanachukulia poa..
Wakiona unasepa ndio wanashituka...
 
Mi wangu kila siku namtumia meseji za mahaba asubuhi ila yeye kimya tu, siku moja nakuta kanitumia sms saa kumi na moja alfajiri nikajua yes na yeye kaanzisha looh kucheki ni rihabari libaya libaya kalicopy mtandaoni kunipestia mimi😂😂 nilichoka aisee!
 
Kwenye Utawala Wangu Maneno Matamu Matamu Sitayasema, Mimi Ni Makavu Tu

Subirini Atakayekuja Labda Atawabembeleza!!
By Mzilankende
 
Back
Top Bottom