Utata Wimbo wa Malaika Nakupenda Malaika

Utata Wimbo wa Malaika Nakupenda Malaika

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
578
Wadau, miongoni mwa nyimbo ziletazo mitafaruku hadi leo ni wimbo huu maarufu uitwao Malaika.
Malaika, nakupenda malaika
Nami nifanyeje, kijana mwenzio
Nashindwa na mali sina
Ningekuoa malaika
Tafadhali sana, mwenye ufahamu kama wimbo huu umeimbwa awali na Mtanzania au Mkenya atujuvye. Naona maelezo ya mtu mmoja kwenye Wikipedia yanampa krediti Mkenya mmoja aitwaye Fadhili. Tujulishane jamani

Asanteni sana
 
Wadau, miongoni mwa nyimbo ziletazo mitafaruku hadi leo ni wimbo huu maarufu uitwao Malaika.

Tafadhali sana, mwenye ufahamu kama wimbo huu umeimbwa awali na Mtanzania au Mkenya atujuvye. Naona maelezo ya mtu mmoja kwenye Wikipedia yanampa krediti Mkenya mmoja aitwaye Fadhili. Tujulishane jamani

Asanteni sana

ni wimbo kutoka EA, inawezekana akawa ni mkenya. Watu wengi wameuiga, Miriam makeba, Boney M

Boney M. - Malaika - YouTube
 
Yasemekana huu wimbo ulitungwa na mtanzania but yule mkenya akawahi kuukatia haki miliki, kutokana na hivyo huu wimbo ni wa yule mkenya kwa sababu ndo anatambulika kisheria
 
Sasa huyo mtanzania hana jina.....km ht jina hajulikani ndo imetoka hiyo tutamtambua fadhili
 
masikini mtunzi! tena inawezekana keshatangulia mbele ya haki hajafaudu ubunifu wake. Shikamoo Tanzania
 
ni wimbo kutoka EA, inawezekana akawa ni mkenya. Watu wengi wameuiga, Miriam makeba, Boney M

Boney M. - Malaika - YouTube

Hakuna aliyeuliza hayo kaka, wengi wanafahamu. Kilichoulizwa ni utata, kama mwimbaji ni Fadhili William au huyo Mtanganyika wa Arusha...
Nyongeza: hata Crazy GK Bokassa a.k.a Amiri Jeshi Mkuu wa East Coast Team, Upanga Mashariki ameimba huwo wimbo akishirikiana na TID Jembe.
 
Mpaka sasa anayejulikana alitunga wimbo huu ni mkenya Fadhili William.Kama kuna mtanzania anafahamika alitunga wimbo huu anayejua aweke jina na ushahidi hapa ili tumfahamu.
 
Hakuna aliyeuliza hayo kaka, wengi wanafahamu. Kilichoulizwa ni utata, kama mwimbaji ni Fadhili William au huyo Mtanganyika wa Arusha...
Nyongeza: hata Crazy GK Bokassa a.k.a Amiri Jeshi Mkuu wa East Coast Team, Upanga Mashariki ameimba huwo wimbo akishirikiana na TID Jembe.

ndio maana nikasema inawezekana ni huyo mkenya. angekuwa ni mtanzania tungeisha mjua. Jifunze kuelewa the whole content ya post na sio kuchukua visehemu nusunusu. Utakuwa umekosea spelling la jina lako spelling sahihi ni mppumbbavu
 
Hizi nyimbo, kuna wimbo unaitwa malaika pia zamani zile ukiimbwa RTD,

"Nimekuja toka Amerika, nimevuka bahari saba, roho yangu inafurahia,roho yangu inafurahia...!"​

Nani anaukumbuka....
 
ukweli kuhusu wimbo huu wa malaika ulitungwa na mtanzania ADAM SALIM mwaka 1945 ulikua ni utunzi kwa ajili ya mpenzi wake
 
Back
Top Bottom