Mmoja wa majeruhi katika shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam juzi, Rubani Francis Shumila amefariki dunia jana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi), alikokuwa akitibiwa.
Wakati hilo likitokea, mama mzazi wa Christine Alfred, binti anayedaiwa kuwa chanzo cha shambulizi hilo, Hellen Alfred amekana kutambua uchumba
Utata wa uhusiano
Ofisa Uhusiano wa MNH, Jacqueline Msuya alisema kuwa amezungumza na mama yake Christine ambaye alimweleza kwamba anatambua kwamba Shumila na mwanaye anayesoma huko Cyprus walikuwa wachumba na kusema kwamba binti yake huyo aliwahi kumwambia kwamba Munisi alikuwa rafiki yake wa kawaida tu.