Utata wa Voda na Jay milioni

Utata wa Voda na Jay milioni

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,493
Reaction score
7,417
Wateja wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania wamehimizwa kujenga utamaduni wa kuacha simu zao zikiwa hewani ili waweze kupata mawasiliano kwa urahisi muda wowote na mahali popote wanapokuwa.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuchezesha droo ya 45 ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo na kufanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo, ambapo mshindi wa pili wa kitita cha shilingi milioni 100 alipatikana. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay au Auto kwenda 15544.

Kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini,Mrisho Millao Wito huo ulitolewa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu wakati wa droo ya 45 ya Promosheni ya Jaymillions ambayo imemuwezesha mmoja wa wateja wa kampuni hiyo kujishindia kitita cha shilingi Milioni 100/- ingawa alipopigiwa simu na maofisa wa kampuni hiyo mbele ya waandishi wa habari na Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha nchini Mrisho Millao simu ya mteja huyo ikawa haipatikani.

"Tunaelewa zipo sababu zisizoweza kuzuilika ambazo zinaweza kusababisha simu ya mteja isiwe hewani lakini vilevile kuna baadhi ya wateja wana utamaduni wa kuzima simu ambao unaweza ukasababisha mteja akose mawasiliano ya muhimu kama mteja wetu huyu leo ambaye tulitaka kumpa taarifa ya kujishindia kitita chake kupitia promosheni yetu ya Jaymillions".

Alisema kwa mjibu wa taratibu za Bodi ya Michezo ya kubahatisha kwa namba hiyo ya ushindi kutopatikana wataendelea kufanya jitihada za kumtafuta mshindi kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia matangazo kwenye vyombo vya habari na kuendelea kumpigia mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili kuona kama kuna wakati atakuwa hewani.

Promosheni ya Jaymillions iliyoanza katikati ya mwezi Januari mwaka huu ambayo itadumu kwa muda wa siku 100 imeleta faraja na itaendelea kuleta faraja na mafanikio kwa wateja wa Vodacom kwa kuweza kujinasua katika hali duni ya maisha na maisha kuwa murua na hadi kufikia sasa wameishapatikana washindi wawili wa milioni 100/-(akiwemo mshindi wa leo),washindi wanne wa Milioni 10/-na washindi 38 wa Milioni 1/-

Nkurlu pia aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni ya Jaymillions katika kipindi hiki ambacho inakaribia kufika mwishoni ili wajishindie kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza bahati zao za kushinda.Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-tu.

Angalizo:
kuna kipindi walidai kuna namba imeshida million mia,wakataja namba 3 za mwisho,wakadai sababu hakucheki amezikosa million mia,Jana tena wameibuka na nyingine kuwa mshindi kazima simu ila hawataji namba ya simu,na hawasemi ilizimwa SAA ngap,kacheki kwa njia hipi outomatic,au katuma msg ya Jay,mda gani alicheki ,tuwe makini watanzania
.
 
Kwanza hawa Voda ukisahau tu hela yako kwenye akaunti ambapo umeacha data za internet on umeliwa, hata uwe na 1000000 utakuta hakuna. Na mpaka uwapate customer care kwa ufafanuzi ni kazi.
 
si kila cku wanatakiwa kutoa hizo hela kwa washindi lkn mbona mambo ni tofauti na matangazo yao
 
Matapeli hao voda,kikawaida kama simu imezimwa ingepaswa kutafuta mshindi mwingine hapo hapo maana kigezo kimojawapo inatakiwa simu iwe hewani unapopigiwa.Niliona hilo nikajua hapa ni usanii full
 
Mimi kila nikiweka fedha wanakata japo sijatuma nena AUTO au JAY MILLIONS. napata sms kwa bahati mbaya umekosa million 100 subiri 10. kwa staili nimeachana na laini ya voda nimechoka kukatwa 900 kila siku ya mchezo usioleweka hauko transparent
 
Mimi kila nikiweka fedha wanakata japo sijatuma nena AUTO au JAY MILLIONS. napata sms kwa bahati mbaya umekosa million 100 subiri 10. kwa staili nimeachana na laini ya voda nimechoka kukatwa 900 kila siku ya mchezo usioleweka hauko transparent

Pole.....
 
Hawana Lolote Wababaishaji Tu Hao Voda,mimi Nilijiunga KWA hiyo'AUTO' lakini hata meseji huwa hawanitumii napesa yangu wamekula!kero tupu.
 
matapeli wakubwa kunasiku yule afisa masoko alisema hatuwezi kuanza kutoa zawadi kwasababu watu hawatumi sms.bahati nasibu ya ukweli ni airtel ambayo mtu hachangishwi sio hawa wahuni
 
Voda ni wezi toka zamani, hakuna mtandao unaibia watanzania kama voda. Hameni huko jaman mnataka mpaka wavunje nyumba zenu ndo mjue wanaiba?
 
Back
Top Bottom