Kuna tabia au mwenendo unaoleta utata wakati wabunge wanapochangiapo mada, makadilio, au miswada ya serikali inayowasilishwa bungeni. Utaona mbunge anapochangia hoja anaanza na kauli " Naunga Mkono Hoja" au atamalizia kwa kauli hiyo huku akionesha kutokubaliana kwa kiasi kikubwa kwa maelezo yake na hoja za serikali juu ya mswada husika.
Hii inaonesha kwamba ushabiki wao kwa chama chao ni mkubwa kuliko mahitaji ya wananchi. Aidha, huwa wakali kwa serikali huku wakijua kwamba hoja wanayoitetea ni ndivyo sivyo. Kesho wakienda kwa wapiga kura wao husema "Niliwatetea na kuwapigania sana bungeni." Je, kuna ukweli wowote hapo.
Je, hakuna dawa ya kurekebisha ugonjwa huu kigeugeu wa wabunge wa CCM.
NAWASILISHA.